August 8, 2016





Simba imeuanza msimu vizuri kwa utambulisho wa kikosi chake kwa kufunga mabao matatu katika mechi moja.

Simba imewatwanga wageni wake AFC Leopards ya Kenya kwa mabao 3-0 katika mechi ya kirafiki maalum katika Simba Day iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji nyota wa Simba, Ibrahim Ajib aling’ara kwa kufunga mabao akianza na dakika ya 38 kwa kushuti kali nje ya 18 kabla ya kuandika la pili katika dakika ya 55.

Simba ilikwenda mapumziko ikiwa na mabao mawili lakini kipindi cha pili, mabadiliko yakaifanya kuwa bora zaidi na kufunga mabao mengine mawili kupitia kwa Shiza Kichuya na Laudit Mavugo akafunga la nne katika dakiaka ya 81.

Ivan Otieno, kipa wa AFC Leopards ndiye alikuwa kipingamizi kikubwa kwa Simba kufunga angalau mabao sita au saba.

Simba inayofundishwa na Joseph Omog raia wa Cameroon, ndiyo ilishambulia kwa kasi zaidi na kuwapa wakati mgumu Leopards waliokuwa wanaongozwa na Raphael Kiongera.

5 COMMENTS:

  1. Sasa Saleh, article ya kwanza Simba walienda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0. Article hii Simba yashinda 4-0! Aya ya kwanza na pili hapo juu, Simba yashinda 3-0 ktk mechi moja! Aya ya nne Simba ilienda mapumziko ikiwa 2-0! Km bao la kwanza lilifungwa dk 38, la pili ni dk ipi na nani kafunga? Mimi nlieko mkoani km naona hizi blog ni useful na live, hizi article ni meaningless! Kizazi nisubi TBC 1?

    ReplyDelete
  2. kwa nini unaandika habari ambayo siyo sahihi? tunaomba mwandishi wa blog hii awe serious na kazi yake, makosa ni kama ifuatavyo:

    1. Simba imeuanza msimu vizuri kwa utambulisho wa kikosi chake kwa kufunga mabao matatu katika mechi moja.

    2.Simba ilikwenda mapumziko ikiwa na mabao mawili lakini kipindi cha pili,

    3. mabadiliko yakaifanya kuwa bora zaidi na kufunga mabao mengine mawili kupitia kwa Shiza Kichuya na Laudit Mavugo akafunga la nne katika dakiaka ya 81.

    HABARI HIZO UKIZISOMA NI KM ZIMEANDIKWA NA MTU ASIYE MAKINI.

    ReplyDelete
  3. Fc leopard wabovu, wapo nafac ya 9 KPL

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic