August 23, 2016

Baada ya kufanikiwa kuitoa Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-1 na kusonga katika hatua ya tatu na ya mwisho kabla ya kufuzu katika michuano ya Afrika kwa vijana, kambi ya timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imevunjwa kwa siku kadhaa kutokana na sababu mbalimbali.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema kuwa sababu ya kuvunjwa kwa kambi hiyo ni kutokana na kuwapa muda wachezaji kupumzika baada ya mechi ngumu, pia walimu wa timu hiyo wanashiriki katika kozi maalum inayoratibiwa na Fifa ambayo inaendelea jijini Dar es Salaam ambayo ilianza tangu jana.



“Kozi hiyo ilianza jana na itaendelea kwa siku tano, hivyo tunatarajiwa wachezaji wa timu hiyo wakapumzike kwa wazazi wao kwa siku hizo walizopewa kupumzika.

“Wachezaji watarejea Agosti 29 kwa ajili ya kujiandaa na safari ya kwenda nje ya nchi kuweka kambi kama ambavyo walivyoahidiwa na uongozi wa TFF na serikali, bado mazungumzo yanaendelea juu ya wapi kambi hiyo itawekwa kwa kuwa tunategemea na mpinzani wetu katika hatua inayofuata.

“Tulitarajiwa kukutana na Congo ambao ndiyo waliowatoa Namibia na tulitakiwa kukutana nao lakini Namibia wamekata rufaa kwa Caf wakipinga mchezaji mmoja wa Congo alikuwa na umri zaidi ya miaka 17, hivyo tunasubiri kuona Cafa wataamua nini,” alisema Lucas.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic