September 13, 2016

Baada ya hivi karibuni kutokea kwa mvutano wa muda mrefu kati ya uongozi wa Azam FC na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusiana na mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba ichezwe uwanja gani hatimaye suala hilo limepatiwa ufumbuzi.

Leo hii hasubu uongozi wa Azam ulikutana na ule wa TFF na kujadili suala hilo na hatimaye kufikia muafaka kuwa mechi hiyo sasa itafanyika katika Uwanja wa Uhuru siku ya Jumamosi.




Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa hapo awali mchezo huo ulipangwa ufanyike kwenye Uwanja wa Taifa lakini kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza hivi karibuni shirikisho hilo likalazimika kuuhamisha Uwanja wa Uhuru.



Amesema TFF imefanya mabadiliko hayo kwa kuzingatia kanuni zake zinazosimamia Ligi Kuu Bara, msimu huu.

“Lakini moja ya sababu kubwa zilizo sababisha hayo yote ni uwanja huo wa Taifa siku hiyo ya Jumamosi kutumiwa na timu ya Taifa ya  vijana ya Congo kwa ajili ya mazoezi yake ya kujiandaa na mchezo wake kuwania tiketi ya kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 dhidi ya Serengeti Boys utakaofanyika Jumapili.


“Timu hiyo inatarajia kuwasili nchini (kesho) leo kwa ajili ya mechi hiyo,” alisema Lucas.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic