September 9, 2016

Unamkumbuka yule kiungo mshambuliaji Mbrazili wa Yanga, Andrey Coutinho? Basi yupo jijini Dar es Salaam baada ya kutua juzi Jumatano kimyakimya.

Kiungo huyo aliondoka Yanga baada ya kusitishiwa mkataba wake wa mwaka mmoja kabla ya kutimkia Rakhine United FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Myanmar barani Asia.

Mbrazili huyo, alisitishiwa mkataba wake ili Mniger, Issofou Boubakar achukue nafasi yake ambaye naye hakudumu na badala yake akatimuliwa baada ya kushindwa kuonyesha kiwango kizuri kabla ya Mzambia, Obrey Chirwa kutua kuziba nafasi hiyo.
 

Coutinho alipotua Dar, juzi.


Coutinho akiwa na mwandishi wa Gazeti la Championi, Wilbert Molandi.

Mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar, Coutinho alipokelewa na mwenyeji wake, Zumo Jumbe ambaye ni wakala wa beki wa pembeni wa Yanga, Juma Abdul na kumpeleka hoteli moja iliyopo Sinza.

Akizungumza na Championi Ijumaa, mara baada ya kutua ‘airport’, Coutinho alisema amekuja nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo na mmoja wa viongozi wa timu hiyo akimficha jina huku akikataa katakata kuweka wazi sababu ya ujio wake.

Coutinho alisema, yeye hivi sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika Agosti 26, mwaka huu, hivyo anaruhusiwa kuichezea timu yoyote itakayomhitaji kwa masharti maalum huku akikataa kabisa kwenda Simba.

Alisema kuwa, kutoka moyoni kwake anatamani kurejea kuichezea Yanga kutokana na mapenzi aliyonayo na yupo nchini kwa siku tano pekee atakazozungumza na kiongozi huyo wa Yanga aliyemuita nchini.

Aidha, Coutinho alisema kingine kitakachomshawishi kurejea Yanga ni aina ya wachezaji waliopo ambao anavutiwa nao ambao ni Mzimbabwe, Thabani Kamusoko na Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.

“Mimi ni mchezaji huru hivi sasa ninayeruhusiwa kusaini mkataba klabu yoyote ikiwemo timu yangu ya Yanga niliyoweka malengo kuwa siku moja nitarejea kuichezea baada ya kujua aina ya soka wanalocheza la nguvu na akili nyingi.

"Hivyo, basi kama ukisikia mimi ninarejea kucheza soka Bongo, basi ninakuja kuichezea Yanga na siyo timu nyingine yoyote na wala usitarajie kusikia ninaichezea Simba, Yanga ni timu kubwa Afrika hivi sasa kutokana na rekodi yao waliyoiweka kwenye michuano ya kimataifa.

“Kwa sasa hivi sifikirii kurudi Asia nilipokuwa nacheza soka la kulipwa kutokana na timu yenyewe kutokuwa na malengo ya ubingwa, pia ina wachezaji dhaifu, mimi ninataka kuichezea timu yenye malengo.

"Nimepanga kukaa nchini kwa siku tano pekee nitakapokuwa na mazungumzo na kiongozi huyo wa Yanga na baada ya hapo nitarejea nyumbani Brazil kwa ajili ya kupumzika, lakini nimepanga kwenda uwanjani kutazama mchezo wa Yanga dhidi ya Majimaji, nimeambiwa wanacheza Jumamosi," alisema Coutinho ambaye amemaliza ligi ya huko akifunga mabao 10.

Aidha, alisema anatarajiwa kwenda kwenye mazoezi ya timu hiyo ili kuwasalimia wachezaji wa Yanga ambao wengi ni marafiki zake.

1 COMMENTS:

  1. Huyo mchezaji Bongo Nzima akuna Anavitu vya pekee Nani Anamuweza Kwa faulo Ndani na Anauxhezaj km Ozil karibi Tanzania kwenye maz3ngwe Atuangali vipaji.Karibu tena Yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic