September 24, 2016





Mabingwa wa Kombe la Chalenji, Kilimanjaro Queens hatimaye wamepewa kipande cha posho zao baada ya kuzisotea kwa zaidi ya saa tano leo.

Wachezaji wa Kilimanjaro Queens wapewa dola 60 tu kila mmoja ambazo ni takribani Sh 130,000 tu kila mmoja. Sasa kila mmoja anadai doka 100 za posho kabla ya ile nyingine waliyoahidiwa baada ya kubeba kombe.

Wachezaji hao kila mmoja alikuwa anadai dola 160 ambazo ni salio la posho zao wakati wakiwa Uganda wakishiriki michuano ya Chalenji na kufanikiwa kubeba ubingwa.

Taarifa za awali zimesema Twiga walipewa posho ya awali ambayo ni dola 100, lakini inaonekana hakuna aliyetarajia kuwaona wakivuka mbele zaidi.

Lakini leo walikaa muda mwingi kwenye ofisi za TFF wakidai fedha zao bila ya mafanikio.

“Kwa kweli wametukatisha tamaa sana, tulidhani wangetudhamini kwamba tumepigana kwa ajili ya taifa. Pia mechi zote za mwishoni wala hatukuwa tumelipwa, lakini hatukusimama wala kuchoka,” alisema mchezaji mmoja wa Kilimanjaro Queens.


Mwingine naye alisema: “Unajua pamoja na juhudi zetu, tunaona suala la tunadhaminiwa vipi, ni kama matangazo. Lakini hali halisi ndani mambo si mazuri, hii si sawa.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic