September 23, 2016


Siku zikiwa zinasonga kwa kasi kuelekea mechi dhidi ya Yanga, Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, amesema anataka kuona washambuliaji wake wanatumia kila nafasi watakayoipata ndani na nje ya 18.

Timu hizo kongwe, zinatarajiwa kuvaana Oktoba Mosi, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Safu ya ushambuliaji ya Simba inaongozwa na Mrundi, Laudit Mavugo, Ibrahim Ajib, Frederick Blagnon huku wakisaidiwa na kiungo mshambuliaji, Shiza Kichuya. 

Omog alisema tayari ameshawaambia wachezaji wake katika hilo, kikubwa anataka kuona timu hiyo inatoka uwanjani ikiwa na ushindi wa aina yoyote.

Omog amesema tayari amewapa mbinu mbalimbali za ufungaji wa mabao kwa njia ya mashuti nje na ndani ya 18, kumchambua kipa na kutumia vema mipira ya krosi na kona kwa ajili ya kupiga vichwa.

“Nitakuwa mkali kwa yule mshambuliaji atakayeleta masihara ya kushindwa kutumia kila nafasi tutakayoipata ndani ya uwanja kwa ajili ya kufunga mabao.

“Kama unavyojua, siku zote bahati haiji mara mbili, hivyo basi ni vema washambuliaji wangu wakaongeza umakini kwa kuitumia vema kila nafasi tutakayoipata tutakapokutana na Simba na timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu.


“Kikubwa nitaka niendelee kukaa kileleni hadi mwisho mwa ligi kuu ili tujiwekee mazingira mazuri ya ubingwa wa ligi kuu, ninavyojua siyo kazi rahisi, lakini tutapambana ili tufanikishe malengo yetu,” alisema Omog.

3 COMMENTS:

  1. hayo kocha unayoyasema ndio muhimu kwa wachezaji kutambua umuhimu wa ligi na club inataka nini sisi mashabiki tunataka furaha

    ReplyDelete
  2. hayo kocha unayoyasema ndio muhimu kwa wachezaji kutambua umuhimu wa ligi na club inataka nini sisi mashabiki tunataka furaha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic