September 19, 2016

Wakati hali ya mambo ikiwa haijakaa vizuri ndani ya Klabu ya Coastal Union ya Tanga ambayo ilishuka daraja msimu uliopita kutoka Ligi Kuu Bara hadi Ligi Daraja la Kwanza, Kaimu Katibu Mkuu wa Coastal Union, Salim Bawaziri, amejiuzulu nafasi hiyo akidai ni baada ya kuona muda wa kufanya hivyo umefika.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Bawaziri alisema ameamua kufanya hivyo baada ya kuona mambo ndani ya kuona mambo ndani ya timu hiyo yanakwenda vizuri na timu ipo chini ya uongozi makini kwa sasa kuliko hapo awali.

Kikosi cha Coastal cha mwaka jana.
“Kama ningeamua kuchukua maamuzi haya hapo nyuma wakati viongozi wa timu hata hawajulikani, ningekuwa sijafanya vizuri na nafsi yangu ingesononeka kwa sababu naipenda Coastal,” alisema Bawaziri.

Bawaziri amesema ameshamwandikia barua mwenyekiti wa klabu hiyo, Ibrahim Twaha lakini hajapata jibu lolote kutoka kwake kwa kuwa hivi sasa yupo kwenye ibada ya hijja jijini Makka, Oman. Hakuna kiongozi yeyote wa Coastal aliyejitokeza kuzungumzia suala hilo.



SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic