September 14, 2016

Hivi karibuni kiungo wa pembeni wa Yanga, Deus Kaseke amekuwa akitumika kama kiungo wa kati wa timu hiyo akichukua majukumu ya Haruna Niyonzima ambapo Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm ameeleza kuhusiana na majukumu hayo huku akitoa sababu za kumzoesha Kaseke kucheza nafasi hiyo.
 

Kaseke (kushoto)


Kaseke ameitumikia nafasi hiyo kwa mechi mbili mfululizo sasa baada ya kukosekana kwa Niyonzima aliyekuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Rwanda. Mechi ya kwanza ilikuwa dhidi ya Ndanda iliyoisha kwa suluhu, ya pili ni ya Jumamosi iliyopita walipoifunga Majimaji 3-0.

Pluijm amekiri kufurahishwa na uchezaji wa Kaseke katika nafasi hiyo ingawa alikuwa na uwanja mpana wa kuchagua viungo wa kati wengine ambao wangeweza kucheza na Mzimbabwe, Thabani Kamusoko eneo la kati.

“Kaseke safi sana, anacheza vizuri akiwa kati, anapambana, anajituma na anajua afanyeje akiwa katika majukumu ya kiungo wa kati. Ndiyo wapo wachezaji wenye uhalisia wa nafasi hiyo ambao ningeweza kuwapanga lakini unaangalia nani anaweza kuziba vizuri pengo kulingana na mfumo,” alisema Pluijm raia wa Uholanzi na kuongeza:

“Kwa baadaye siwezi kujua kama Kaseke anaweza kuhamia katika nafasi hiyo moja kwa moja lakini ni jambo muhimu kumzoesha mchezaji kama huyu ambaye anaweza kusimama nafasi mbalimbali na akacheza kwa asilimia kubwa au kuliziba kabisa tatizo.”

Katika majukumu yake hayo mapya, Kaseke alifanikiwa kufunga bao moja juzi katika mechi ya Majimaji likiwa ni bao lake la pili msimu huu baada ya awali kufunga dhidi ya African Lyon.

 SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic