September 24, 2016

MPIRA UMEKWISHAAAA
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 88 hadi 89, Simba wanaonekana kumiliki mpira zaidi na Majimaji wanafanya kazi ya kuokoa
Dk 86, Bukungu anapiga shuti kali kabisa, lakini Amani Simba imara anapangua
GOOOOOO Dk 81, Kichuya anaifungia SImba bao la nne na lake la pili leo baada ya mabeki wa Majimaji kudhani ameotea
SUB Dk 80, Majimaji wanamuingiza Tarick Simba kuchukua nafasi ya mshambuliaji wao tegemeo Selemani Kibuta
GOOOOOOO Dk 75, Mnyate anaifungia Simba bao safi la tatu baada ya Mohammed Ibrahim kuwatoka mabeki watatu wa Majimaji
Dk 72, Krosi safi ya Bukungu, Mnyate anapiga kichwa maridadi lakini Amani Simba anaokoa kwa ustadi mkubwa na kuwa kona ambayo haina madhara
Dk 70, Amani Simba anafanya kazi ya ziada, anaokoa shuti kali la Said Ndemla, konaaa...inachongwa na Kichuya, anaokoa tena Amani na kuwa kona nyingine, inachongwa tena, anadaka kwa umaridadi mkubwa
GOOOOOOOOOO Dk 66, Kichuya anapiga penalti safi kabisa akimuangusha kushoto kulia Amani Simba na kuandika bao la pili kwa Simba
PENAAAAALT DK 65, Marcell anaushika mpira na mwamuzi anasema ni penaaaalt

Dk 63, Kichuya yuko chini anatibiwa, haijajulikana nini tatizo....inaonekana aligongwa na mpira uliotokana na shuti la Marcell
SUB Dk 62, Simba wanamtoa Mavugo na nafasi yake inachukuliwa na Ame Ali
SUB Dk 60, Majimaji wanamtoa Luka Kikoti na nafasi yake inachukuliwa na kinda wa zamani wa Simba, Marcell Boniventura
Dk 55, Mohammed Ibrahim naye katika nafasi nzuri, anapiga mpira unaombabatiza Lulanga
Dk 54, anapoteza nafasi nzuri kabisa baada ya Amani Simba kutoka na yeye kupiga shuti la chinichini, lakini halikulenga lango
Dk 53, Majimaji wanasukuma shambulizi na kupata kona lakini inakuwa haina matunda kwao
SUB: Dk 50, Simba wanamtoa Mzamiru, nafasi yake inachukuliwa na Mohammed Ibrahim
Dk 49, hadi sasa hakuna timu iliyofanya shambulizi kali
Dk 46, Mpira umeanza na inaonekana hakuna shambulizi kubwa, kila upande ukionekana kuvizia


MAPUMZIKO
-Mwamuzi Rudovick Charles kapuliza kipenga kuashiria ni mapumziko
-Kipa wa Amani Simba, yuko chini akipatiwa matibabu
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, Mavugo anawalamba chenga mabeki wa Majimaji lakini shuti lake linakuwa mtoto kabisa
Dk 38 hadi 42, mpira unaonekana umepunguza kasi kwa kiasi kikubwa kabisa
Dk 36, krosi safi ya Mohamed Zimbwe, inamkuta Mzamiru anapiga vizuri kabisa lakini hakulenga lango

Dk 34, Mavugo anaingia vizuri kabisa katika eneo la hatari, lakini anajaribu kufunga katika eneo ambalo angeweza kutoa pasi
Dk 33, Kichuya anaukwamisha mpira wavuni, lakini mwamuzi msaidizi, Mugando anasema alikuwa ameishaotea
Dk 32, nafasi nzuri kabisa ya kwanza ya Majimaji, George Mpole akiwa amebaki na kipa wa Simba, anashindwa kulenga lango
Dk 31, Kichuya anapiga shuti la mpindo, lakini Amani Simba anakuwa makini na kuokoa kwa umakini kabisa
SUB Dk 25, Ndemla anaingia kuchukua nafasi ya Ajibu
Dk 24, Kichuya anapoteza nafasi nzuri baada ya kupaisha shuti juu karibu na lango la Majimaji

Dk 22, Ajib anakwenda nje baada ya kuumia, inaonekana nafasi yake itachukuliwa na Said Ndemla
Dk 21 mpira unasimama, Ajib yuko chini akipatiwa matibabu
Dk 19, Simba wanafanya shambulizi tena, Mnyate anaingia vizuri kabisa lakini mabeki wanaokoa vizuri kabisa
Dk 14 hadi 16, Simba, Majimaji pia wanagongeana mpira katikati ya uwanja zaidi
Dk 13, Ajibu anamtoka Hamad Kipobile na kupiga shuti la chinichini lakini linatoka sentimeta chache nje ya lango la Majimaji, Amani Simba anawalaumu mabeki wake hapa

Dk 12 krosi safi ya Mnyate lakini inakosa mtu, Majimaji wanachukua na kuanza kugongeana lakini wanatuliza mpira kwa kucheza taratibu
Dk 10, shambulizi la kwanza la Majimaji lakini Mollel anachelewa kuuwahi mpiga na kipa Vicent wa Simba anawahi na kudaka

Dk 8 hadi 9, Simba wanaonekana kushusha presha na kugongeana taratibu
Dk 7, Simba wanagongeana vizuri na kuingia hatari kabisa, lakini Lulanga Mapunda anaokoa na kuwa kona, Simba wanaichonga lakini haina matunda
GOOOOOO Dk 4, Jamal Simba Mnyate anaipatia Simba bao la kwanza baada ya krosi safi ya Mavugo, Ajib akapiga shuti la chini lakini kwa ulaiiiniii Mnyate anamalizia baada ya kipa Amani Simba, kupangua

Dk 2, Simba wanapaleka shambulizi jingine baada ya Majimaji kushambulia lakini bado linakuwa dhaifu
Dk ya 1, mechi imeanza kwa kasi kubwa na Simba wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Majimaji, lakini ni offside.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic