September 18, 2016


Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka Serengeti Boys imepata ushindi wa mabai 3-2 dhidi ya Congo Brazzaville katika hatua ya tatu kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa vijana itakayofanyika mwakani.

Mchezo huo ambao ulifanyika kwenye Uwanja wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ulishuhudiwa na maelfu ya mashabiki ambao waliingia bure uwanjani hapo kutokana na agizo la Waziri Nape Nnauye, aliyetaka iwe hivyo ili kuwoangezea nguvu Serengeti Boys.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakamilika Serengeti ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0, yakiwa yamewekwa wavuni na Yohana Mkomola katika dakika ya 39 na 42.

Baada ya kufunga bao la pili alishangilia kwa kuvua jezi yake jambo ambalo lilisababisha apewe kadi ya njano.
Dakika ya 72, Congo walipata penalti baada ya mchezaji wao mmoja kufanyiwa faulo ndani ya eneo la 18, wakapiga na kufunga, dakika ya 82, Serengeti walipata bao la tatu kupitia kwa Issa Makamba na kuamsha shangwe.

wakati Watanzania wakiamini timu yao imeshinda mabao 3-1, Wacongo hao walipata bao la pili katika dakika ya 90 baada ya mabeki wa Serengeti kujisahau.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2 ambapo mshindi wa hapo atasonga mbele kwa kufuzu moja kwa moja katika michuano hiyo ya vijana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic