September 15, 2016

Manchester United ikiwa na wachezaji wapya nane kwenye kikosi cha chake kilichocheza mchezo wa wikiendi iliyopita dhidi ya Manchester City, Alhamisi hii ilishindwa kufurukuta na kujikuta ikilala kwa bao 1-0 dhidi ya Feyenoord.

Kipigo hicho kimekuwa kama mshtuko kwa mashabiki wengi wa timu hiyo kutoka Jiji la Manchester ambao waliamini ni mchezo mwepesi kwa timu yao kupata ushindi.

Huo ulikuwa mchezo wa kwanza wa United wa Kombe la Europa kwenye Dimba la De Kuip baada ya kukosa nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kocha Jose Mourinho alimweka nje mshambuliaji wake hatari Zlatan Ibrahimovic na kuanzisha kikosi chenye wachezaji wengi ambao hawapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza na ilipofika dakika ya 78, Fayenoord walifanikiwa kujipatia bao lao kupitia kwa Van der Heijden kwa shuti kali.

Feyenoord ambao mashabiki wake walikuwa wakishangilia kwa dakika zote 90 walionyesha kiwango cha juu ambapo walikuwa na kasi kubwa kuanzia kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili, United ambao wamefungwa mchezo mmoja tu kati ya minne ya Ligi Kuu England walianza kwa kasi lakini ukuta wa wenyeji hao ukawa mgumu kupitika.

Dakika ya 60, Mourinho alifanya mabadiliko kwa kumtoa Marcus Rashford na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahimovic, huku Juan Mata akitoka na kuingia Ashley Young ambao waliongeza kasi kwenye safu ya ushambuliaji ya United lakini bado hawakusaidia kitu.

Mashabiki wa Uholanzi walimzomea Ibrahimovic muda mwingi wa mchezo kwa kuwa aliwahi kuwachezea wapinzani wao, Ajax.









Kwa upande wa timu ya Genk ambayo anaichezea Mtanzania Mbwana Samatta, wenyewe walifanikiwa kufanya mambo makubwa kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0, lakini kibao kikageuka kipindi cha pili na kulala kwa mabao 3-2 dhidi ya Rapid Wien hadi dakika 90 zinamalizika.

Samatta alikuwa akiongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ambayo ilijipatia mabao yao kupitia kwa Bailly aliyefunga dakika ya 29 na dakika ya 90 kwa mkwaju wa penalti.

Matokeo mengine ya michuano hiyo ya Europa iliyopigwa leo usiku:

Matokeo mengine
Anderlecht 3-1 Gabala, APOEL 2-1 Astana, Astra 2-3, Austria Vienna, AZ Alkmaar 1-1 Dundalk, Maccabi Tel Aviv 3-4, Zenit St Petersburg, Mainz 1-1 St Etienne, Plzen 1-1 Roma, Sassuolo 3-0 Athletic Bilbao, Young Boys 0-1 Olympiacos, Zorya 1-1 Fenerbahce.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic