September 14, 2016

Kocha wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm amefunguka kwamba hapendezwi na aina ya pasi nyingi zisizo na faida zinazopigwa na viungo wake Thaban Kamusoko na Deus Kaseke jambo ambalo linachelewesha ushindi kwenye mechi zao.

Mholanzi huyo tayari ameshaiongoza Yanga kushinda mechi mbili na sare moja huku wakijikusanyia pointi saba ambapo kwenye mchezo wao uliopita, aliwatumia Kamusoko kwenye kiungo wa ukabaji na Kaseke kwenye kiungo cha uchezeshaji.





Pluijm ambaye aliwahi kuinoa timu ya Berekum Chelsea ya Ghana, amelieleza gazeti hili kwamba anakerwa na pasi nyingi ambazo zinapigwa na viungo hao, hasa nyingi zikiwa za nyuma bila ya kwenda eneo la mpinzani jambo ambalo linawafanya kumiliki mpira kwa muda mrefu huku likichelewesha wao kushinda.

“Sikatai kwamba tunatakiwa kucheza soka la kuvutia lakini muda mwingine soka hilo halina umuhimu sana unaposaka matokeo kwani kumiliki mpira hakukupi pointi tatu na badala yake mabao utakayofunga ndiyo kila kitu.

“Tatizo letu ni kwamba tunapiga sana pasi lakini zote hizo zinakuwa kwenye eneo letu, nyingi zikiwa za nyuma kuanzia kwa mabeki na viungo, jambo ambalo kwangu naona halina maana sana kwani hatufaidiki na wingi wa pasi hizo ambazo tunacheza kwetu tu,” alisema Pluijm.

 SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic