September 21, 2016



Timu ya taifa ya vijana chini  ya miaka 17, Serengeti Boys inatarajia kuondoka nchini kesho Alhamisi kuelekea Rwanda, kuweka kambi ya muda mfupi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Congo Brazzaville utakaochezwa Oktoba 2, mwaka huu.

Serengeti ipo katika hatua ya mwisho ya kuwania tiketi ya kushiriki fainali za vijana chini ya umri wa miaka 17 zitakazofanyika Madagascar, mwakani kufuatia kubakiwa na mchezo wa marudiano  dhidi ya Congo ambayo katika mchezo wa awali waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 .

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema, awali benchi la ufundi lilipendekeza kambi iwe Madagascar lakini TFF imeonelea ni vyema wakaenda Rwanda ambapo ni karibu zaidi ikiwa ni pamoja na usafiri wake kutumia  saa machache tofauti na walipokuwa wakipahitaji.

“Serengeti itaondoka nchini siku ya Alhamisi kuelekea Rwanda na itakaa huko hadi muda wa kwenda Congo utakapofika na wataondokea hukohuko, kikosi kwa ujumla kipo vizuri.

“Awali benchi la ufundi lilipendekeza kwenda Madagascar lakini tumeona ni vyema waende huko kwa kuwa ni karibu zaidi ya walikokuwa wanakuhitaji pia hakutumii  muda mrefu,” alisema Alfred.


Alimalizia  kwa kusema kuwa, Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza, itaanza kutimua vumbi Jumamosi hii ambapo timu 24, zinashiriki na vituo vitakuwa vitatu vikiwemo Mlandizi, Majimaji, Songea na Mkwakwa, Tanga, pia ameeleza ligi ya wanawake itaanza kutimua vumbi Oktoba 4, kwa timu 12 kushiriki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic