September 16, 2016

Wakati homa ya pambano kati ya Azam FC dhidi ya Simba litakalopigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru, badala ya Uwanja wa Taifa ikizidi kupanda, Simba haijafurahishwa na maamuzi hayo, imeripotiwa kuwa wamekuwa wakifanya bidii kushawishi mabadiliko ya uwanja.

Mchezo huo ambao Azam FC ndiyo wenyeji, ulipangwa kufanyika Taifa lakini kutokana na uwanja huo kutumiwa na timu ya taifa ya vijana ya Congo Brazzaville (U-17) kesho Jumamosi kufanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezo dhidi ya Serengeti Boys, Jumapili kama sheria ya Fifa inavyosema, ikalazimu kufanyika kwa mabadiliko hayo.



Inadaiwa kuwa Simba inahofia kupoteza mchezo huo kwa kuwa wachezaji wao bado hawajazoea nyasi za Uwanja wa Uhuru ambazo ni za bandia wakati Azam wao wanao uwanja wa nyasi bandia.

Hadi jana Alhamisi jioni viongozi kadhaa wa Simba walikuwa wanafanya kila liwezekanalo kuishawishi Congo kuutumia Uwanja wa Taifa, leo Ijumaa kwa mazoezi ya mwisho badala ya kesho ili waweze kuutumia.

Aidha, mtu wa ndani wa TFF amelithibitishia Championi Ijumaa kuwepo kwa kampeni hiyo ya Simba kwani wanajua nyasi bandia ni faida kwa Azam ambao wamezoea nyasi hizo kuanzia mazoezini mpaka kwenye mechi nyingi.

“Lakini sidhani kama mpango wao unaweza kukubalika kwa muda uliobaki na sidhani kama Congo wenyewe wanaweza kuwakubalia.

“Kumbuka wamekuja kucheza mechi ya mwisho kufuzu Fainali ya Mataifa Afrika, siamini kabisa,” alisema kigogo mwenye hadhi kubwa ndani ya TFF.

Alipotafutwa  Mratibu wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’ alisema: “Sina hizo taarifa na kazi yangu ni kuiandaa timu kuona inafanya vizuri. Kama ni maamuzi ya kutupeleka Uwanja wa Uhuru sisi tumeridhika.”



SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic