September 3, 2016


BUKUNGU ALIPOTUA SIMBA RASMI


Kocha wa Simba, Joseph Omog amesema kukosekana kwa bekiBesala Bukungu na kiungo Mousa Ndusha kumeharibu mipango yake kikosini.

Bukungu na Ndusha ambao wote ni raia wa DR Congo, wameshindwa kuitumikia Simba kutokana na kukosa hati zao za uhamisho (ITC).

Wachezaji hao ambao wamesajiliwa hivi karibuni, mpaka sasa wanasotea kusaka ITC zao ambazo zimeelezwa bado hazijawafikia na kuwafanya kushindwa kucheza michezo miwili ya Ligi Kuu Bara tangu msimu ulipoanza Agosti 20, mwaka huu.

NDUSHA ALIPOTUA SIMBA RASMI
Mpaka sasa Simba imeshacheza mechi mbili, imeshinda moja dhidi ya Ndanda FC na imetoka sare na JKT Ruvu. Katika nafasi ya Bukungu wapo Hamad Juma, Malika Ndeule wakati kwa Ndusha yupo Mzamiru Yassin.

Akizungumzia ishu ya kushindwa kuwatumia wachezaji hao mpaka sasa kutokana na matatizo hayo, Omog aliliambia Championi Jumamosi:“Inanihuzunisha sana kuona wachezaji wangu Bukungu na Ndusha hatuwatumii kutokana na kukosa ITC, hao wote walikuwa kwenye mipango yangu na kukosekana kwao kumeniharibia.

“Ukiangalia, kwa mfano Bukungu nilikuwa namtegemea kusaidia zaidi kwenye safu ya ulinzi upande wa kulia, lakini hatuwezi kumtumia kwa sasa na nalazimika kufanya jitihada za kutafuta mbinu nyingine bila uwepo wao.”


Msimu uliopita, Simba ilimsajili Danny Lyanga kutoka FC Lupopo ya DR Congo, lakini alishindwa kuitumikia timu hiyo baada ya ITC yake kuchelewa hadi wakati wa usajili dirisha dogo ilipoletwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic