October 20, 2016




MPIRA UMEKWISHA
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
GOOOOOOOO Dk 86, krosi ya Bukungu, Blagonon anatoa pasi safi ya kichwa kwa Muzamiru ambaye anaandika bao safi kabisa


Dk 83, Simba wanafanya shambulizi tena lakini Blagnon anachelewa. Bado Simba wanaonekana kupania kufunga kwa kuwa wanaonana vizuri
Dk 74 hadi 79, Mbao wanaonekana kupoteza mwelekeo na kutoa nafasi nyingi za mashambulizi kwa Simba
Dk 71, mpira wa adhabu wa Kichuya unatua kwa Mkude, lakini anashindwa kulenga lango
Dk 68, Mbao wanashambulia kwa kasi lakini piganikupige, Simba wanaokoa
Dk 65, Mo Ibrahim anawahadaa walinzi wa Mbao, anaingia vizuri lakini shuti lake nyanya
SUB Dk 63, anatoka Hussein Sued anaingia Frank Damas upande wa Mbao
Dk 60, Blagnon anaunawa mpira na kufunga, lakini mwamuzi anashitukia dili
Dk 58 hadi 63, Simba wanaonekana kuutawala mchezo zaidi lakini zaidi ni katikati ya uwanja
SUB Dk 58, Simba wanamtoa Ajibu na nafasi yake inachukuliwa na Mohamed IbrahimDk 56, Kazimoto naye anaingia vizuri na kupiga shuti kali kabisa
Dk 55, nafasi nzuri kabisa ya Simba Kichuya anapiga shuti kuubwa linapita juu ya lango la Mbao FC
SUB Dk 50, Simba wanamtoa Mavugo na Frederick Blagnon anaingia
Dk 47 Mechi imeanza kwa kasi kila upande ukionekana umepania kushinda bao la mapema

MAPUMZIKO
-Mbao wanaonekana kulinda zaidi wakitaka kwenda mapumziko na sare

DAKIKA 1 YA NYONGEZA
Dk 44, Simba wanapata kona nyingine, Mavugo anajaribu, Mbao wanaokoa na kuwa kona tena
Dk 41, nafasi nyingine kwa Simba, Mavugo anaachia shuti lakini anashindwa kulenga lango
Dk 39, Ajib anamtoka beki wa Mbao na kuachia shuti kali lakini kipa anaokoa tena
Dk 36, Sued anaachia shuti kali, mpira unamgonga Angban tumboni na kuwa kona hata hivyo inakuwa hana faida kwao
DK 34, Kichuya anachonga kona nzuri lakini kipa wa Mbao anaendelea kuonyesha umahiri wake

Dk 30, Sued anaingia vizuri lakini pasi nzuri alitoa inakosa mtu na Simba wanaokoa 
Dk 24 hadi 28, Simba ndiyo wanamiliki mpira zaidi, lakini hawako makini wanapofika langoni
Dk 23, Mavugo anageuka na kuachia shuti kali, kipa Mbao FC anaokoa tena na kuwa offside

Dk 21, shambulizi la kwanza kubwa la Mbao FC, Hussein Sued anaingia lakini anagongana na kipa Angban
Dk 21, nafasi nyingine kwa Simba, Muzamiru anapiga shuti kali kabisa hapa, lakini goal kick
Dk 19, Bukungu anapiga krosi safi kabisa, Mavugo anapiga kichwa lakini kipa wa Mbao anadaka kwa ufundi kabisa hapa
Dk 16, Simba wanafanya shambulizi kali, Mavugo anaingia anageuka na kuingia ndani na kupiga shuti kali, kipa anaokoa mpira unamkuta Ajib anapiga shuti linagonga mwamba na kutoka nje

Dk 11, Simba wanaonekana kutawala mpira, lakini Mbao FC si timu ya kubeza kwa kuwa wanajibu mashambulizi
Dk 8, Mkude anapigashuti kali kabisa, mabeki wanaokoa na kuwa kona
Dk 5, nafasi nyingine nzuri kwa Simba, lakini Kichuya anapiga shuti linapaaa juu
Dk 3, Mavugo yeye na kipa, anapoteza nafasi nzuri kabisa ya kufunga baada ya kuukosa mpira wa kichwa
Dk 1, mechi kati ya Mbao FC wageni wa Simba, imeanza taratibu huku kila upande ukionekana kujipanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic