October 30, 2016






MPIRA UMEKWISHA
-Mbao wanapata kona baada ya Bossou kuutoa mpira, inachongwa lakini Yanga wanaokoa
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
KADI Dk 88, Kipa Dida analambwa kadi ya njano kwa kuchelewesha mpira kwa makusudi
Dk 87 sasa, Mbao wanaonekana kuamka na kutaka kupata bao angalau moja, lakini bado Yanga wako vizuri zaidi
Dk 84 sasa, Yanga wanaonekana kuupoza mchezo huku Mbao kama wamekata tamaa ingawa mara kadhaa wanajitahidi kushambulia
Dk 80 Ndikumana anapiga mkwaju wa adhabu hapa, lakini Dida anadaka kwa ulaini kabisa
Dk 78 sasa, kwa hali ilivyo, Mbao wanaonekana kupoteana kabisa, Yanga wanapiga pasi wanavyotaka. Lazima Mbao FC waimarishe uchezaji wao kwenye kiungo, la sivyo Yanga wanaweza kushindilia bao la nne

GOOOOOOOOO Dk 75, Tambwe anaifungia Yanga bao safi kabisa akiunganisha pasi safi ya Simon Msuva
DK 74, Donald Ngoma anaruka na kupiga kichwa mpira wa kurusha wa Twite, lakini safari hii kipa yuko makini
SUB Dk 71, Yanga wanamtoa Chirwa na nafasi yake inachukuliwa na Donald Ngoma
KADI Dk 70 Ndikumana analambwa kadi ya njano kwa kumkwatua Haji Mwinyi
SUB Dk 64, Yanga wanamtoa Hassan Kessy na nafasi yake inachukulwia na Thabani Kamusoko, maana yake Mbuyu Twite anakwenda pembeni kulia
Dk 62, Tambwe anaachia kombora hapa linagonga mwamba na kutoka nje, ilikuwa ni al manusura
SUB Dk 56, Juma Mahadhi anaingia kuchukua nafasi ya Kaseke

GOOOOOOOOOO Dk 55, mpira wa kurusha wa Twite unakwenda moja kwa moja kwa moja wavuni kipa kuupangulia ndani
SUB Dk 54 Venance Ludovic anaingia Damas Msiba kwa upande wa  Mbao FC
Dk 50, Yanga wanazidi kusukuma mashambulizi, Niyonzima anaangushwa hapa, anatibiwa
GOOOOOOOOO Dk 49, Bossou anafunga bao lakini mpira unagusa mkono wake kabla ya kuingia wavuni. Ilikuwa ni baada ya kuunganisha krosi ya Niyonzima aliyepiga mpira wa adhabu 
Dk 46, Yanga wanaanza kwa kasi wakishambulia zaidi na wanaonekana wanataka bao la mapema

MAPUMZIKO

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, Tambwe anapokea pasi nzuri ya Niyonzima na kupiga vizuri lakini mpira unatoka kiduchu kabisa
SUB Dk 42, Salum Sued anakwenda nje kwa upande wa Mbao FC, nafasi yake inachukuliwa na Maganga
Dk 37, Bado hakuna hata shambulizi kubwa. Inaonekana wazi Yanga wanahitaji mtu wa kulazimisha kama Ngoma vile. Chirwa na Tambwe wanaonekana 'kutoiva' pamoja
Dk 30, bado inaonekana hakuna shambulizi kali zaid ya kona. 
Dk 24, Mbao wanapata kona baada ya Bossou kulazimika kutoa nje mpira, inachongwa lakini Dida anadaka vizuri kabisa

Dk 18, Yanga inapata kona ya kwanza baada ya beki Mbao kumuwahi Msuva na kuutoa. Inachongwa lakini haina manufaa
Dk 14, hakuna shambulizi kali kwa upande wowote, inaonekana kila upande bado haujajipanga katika umaliziaji
Dk 8, Chirwa anapiga shuti kimo cha nyoka lakini linatoka sentimeta chache kabisa nje ya lango la Mbao
Dk 6, krosi safi ya Kaseke, Msuva anaunganisha vizuri kabisa lakini anashindwa kulenga lango. Yanga imetumia takribani dakika nne ikigongena vizuri kabisa
Dk 1 mpira unaanza taratibuuu kila upande unaonekana ukiwa makini kwa kutaka kufunga na kuepuka kufungwa

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic