October 8, 2016



Unaona, sasa jamaa ana bao moja tu katika mechi saba za Ligi Kuu Bara, lakini sasa straika wa Simba, Frederic Blagnon ameingiwa na hofu juu ya kiwango chake kwani ameambiwa mikoani kuna viwanja vibovu.

Blagnon aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea kwao Ivory Coast, hajawahi kucheza mechi ya ligi kuu nje ya Dar es Salaam kwani alikuwa ‘anakula raha’ kwenye viwanja vya Taifa na Uhuru.

Straika huyo amesema amepewa taarifa za hali ya ubovu wa viwanja vingi vya mikoani, hivyo anahofia kiwango chake kitashuka na amewaomba mashabiki wamvumilie tu.

“Nimesikia tunapoenda huko mikoani viwanja si vizuri, hii inanitia wasiwasi kwani hapa tunapofanyia mazoezi tu si pazuri na napata shida, sasa itakuwaje tukienda huko kucheza mechi?

“Nitajitahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha naisaidia timu yangu, hivyo naomba mashabiki wasinielewe vibaya pale nitakaposhindwa kufunga mimi hapa ni mgeni na sijazoea,” alisema Blagnon.

Ili kuzoea mapema hali watakayokutana nayo kwenye Uwanja wa Sokoine jijini watakapocheza na Mbeya City Jumatano ijayo, Simba wiki hii imekuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Kinesi uliopo Urafiki na Uwanja wa Polisi, Kurasini, vyote vya jijini Dar es Salaam.

SOURCE:CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic