October 1, 2016


MSUVA
Beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’, maarufu kama Tshabalala, amesema ataweka ulinzi mkali kwa mawinga wa Yanga wasipite kwake leo, lakini Simon Msuva amesema atapita hukohuko katika upande wake.

Yanga na Simba zinacheza leo mchezo namba 43 wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo tayari Tshabalala ameshapiga mkwara kwamba hataruhusu mtu kupita upande wake.

Kwa upande wake, Msuva ambaye ni winga anayemudu kucheza upande wa kulia, alisema: “Nimemsikia Tshabalala akitamba kuwa hatuogopi, mimi namwambia tutaonana uwanjani.
ZIMBWE JR
“Ninaamini nitafanya kazi yangu kama kawaida na nitapitia hukohuko alipo yeye (Tshabalala) kwani nimefanya mazoezi makali kujiandaa na mchezo huu.”

Msuva alisema hapendi kumzungumzia mchezaji wa timu pinzani, lakini amelazimika kutoa kauli hiyo kwa Tshabalala ili kuwatoa hofu mashabiki wa Yanga wanaodhani anaweza kuzuiwa na beki huyo.


“Tshabalala yeye kama anaongea hivyo, mwacheni tu, lakini kikubwa anatakiwa kutambua kuwa soka linachezwa uwanjani na siyo mdomoni,” alisema Msuva ambaye hadi sasa ana bao moja katika ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic