October 28, 2016



Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ameweka hadharani kilichomkasirisha Kocha Hans van der Pluijm hadi akaamua kuachia ngazi kuinoa Yanga.

Mwigulu ambaye ni shabiki mkubwa wa Yanga, ndiye aliyekutana na Pluijm na kumshawishi kubadili uamuzi wake wa kubwaga manyanga kuinoa Yanga.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, kiongozi huyo na kada wa CCM, amesema Pluijm alikasirishwa na Yanga kumleta kocha George Lwandamina wakati yeye akiwa bado kazini.
“Alikarishwa na hilo, aliona analetwa kocha mwingine. Aliponieleza, nikazungumza naye na kumshawishi kubadili uamuzi wake.
“Lakini nilipozungumza na uongozi wa Yanga, nao wakaonekana hawakuwa na tatizo hata kidogo na wanamheshimu sana kocha.
“Kikubwa nimeona kama Yanga wanataka kufanya mabadiliko, wanaweza kufanya hivyo hapo baadaye, mfano wakati wa mapumziko na si sasa katikati ya ligi.
“Tena utaona kocha waliyenaye anafanya vizuri, amefanya vizuri kwa kuchukua makombe yote msimu uliopita,” alisema Mwigulu.
“Mwenyekiti (Yusuf Manji), hata yeye alisema haikuwa sahihi kocha ambaye ameweka heshima Yanga kuondoka kwa staili hiyo. Hivyo mwisho tumeafikiana na yeye ataendelea na kazi.”
Mara baada ya kutua kwa Lwandamina, Pluijm aliamua kuachana na Yanga kwa kuandika barua ya kubwaga manyanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic