October 10, 2016


NYONI

Viongozi wa benchi la ufundi la Azam FC sasa wanapumua kwa raha zao kutokana na mabeki wao wawili muhimu kurejea uwanjani.

Tangu kuanza kwa michuano ya Ligi Kuu Bara msimu huu, timu hiyo ilikosa huduma ya mabeki wake wa kutumainiwa, Erasto Nyoni, Pascal Wawa na Aggrey Morris ambao walikuwa wakisumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu.

Hivi sasa nyota hao wamepona na tayari wameanza kuitumikia timu hiyo ambapo hivi karibuni walicheza mechi ya kirafiki wakijumuishwa na kikosi cha vijana na wakaonyesha kiwango cha juu, jambo ambalo liliwafurahisha viongozi wa benchi la ufundi la Azam.

Kutokana na hali hiyo, kocha mkuu wa timu hiyo ambayo imekuwa na mwendo wa kusuasua, Mhispania, Zeben Hernandez, amedai kuwa kurejea uwanjani kwa wachezaji hao ni habari nzuri kwake kwani ile hofu aliyokuwa nayo sasa imeondoka na anatarajia makubwa katika mechi zijazo za timu hiyo.

“Nimevutiwa na uwezo wao walioonyesha katika mechi hiyo ya kirafiki, hivyo kuanzia sasa naweza kuanza kuwatumia katika mechi zetu zijazo, kwani kutokuwepo kwao katika kikosi changu, lilikuwa ni pengo kubwa sana,” alisema Harnandez.

Azam hivi sasa inashika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi kuu, ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza mechi saba na kufanikiwa kushinda tatu, sare mbili huku ikifungwa pia mechi mbili.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic