October 6, 2016

RUNYETA
Ule mfumo wa elektroniki uliokuwa ukipingwa na watu wengi hasa wale wapigaji, umefanikiwa baada ya kwisha kwa mechi ya watani Yanga dhidi ya Simba.

Kampuni ya Selcom Tanzania ndiyo waliyopewa tenda ya kusimamia mfumo wa tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Taifa na Uhuru jijini Dar na wamesema kweli mambo yameenda safi kabisa.

Hata hivyo, wamekili kwamba kulikuwa na changamoto kadhaa ambazo zinaendelea kufanyiwa kazi.

Meneja Miradi wa Selcom, Gallus Runyeta amesema wanaamini katika mechi zijazo, mambo yatakuwa safi kabisa.

"Kila kitu huanza taratibu, changamoto ni jambo la kawaida. Lakini mafanikio yamekuwa makubwa sana. Tumefanikiwa kwa asilimia 62, tunaamini itakwenda inapanda kadiri siku zinavyosonga mbele," alisema Runyeta alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Taifa, leo.



“Unajua watu walikuwa wakikosea namna ya kuingia uwanjani kwa utaratibu na ndiyo maana mfumo uligoma, hapa katika hizi mashine anatakiwa awe amesimama mtu mmoja na sio zaidi ya hapo, wakizidi tu mfumo haufanyi kazi, na hicho ndicho kilichotokea siku ile, watu walijazana sana karibu na mashine.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic