October 12, 2016



Katika kile kinachoonekana ni kuiwekea kizingiti Yanga inayomnyemelea kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Charles Mkwasa, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemkabidhi gari kocha huyo ikiwa ni sehemu ya kumshawishi aendelee kuwa nao baada ya juzikati kutishia kutoongeza mkataba.

Wiki kadhaa nyuma, Mkwasa alijitutumua na kuanika ‘uozo’ unaoiua Taifa Stars kutofanya vizuri, moja ya matatizo hayo akisema ni kukosa fursa ya kuangalia vipaji vya wachezaji mikoani, badala yake amekuwa akiishia kuangalia mechi zinazochezwa jijini Dar es Salaam ili kupata kikosi cha Stars na kuhitimisha kuwa huenda akabakia kuwa mshauri na si kuendelea na ukocha kikosini hapo baada ya Machi, mwakani.

Na taarifa za motomoto ni kuwemo kwa mpango wa Yanga kumnyemelea chinichini ili kumrejesha kikosini, hata hivyo TFF ni kama imeshtukia mpango huo na kumkabidhi gari aina ya RAV 4, maalum kwa ajili ya kwenda mikoani kuangalia mechi mbalimbali za ligi kuu na ikiwezekana daraja la kwanza.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas, amesema ishu hiyo na kwamba tayari ameishaanza ziara zake, akianzia mkoani Pwani wikiendi iliyopita katika mchezo kati ya JKT Ruvu na Mtibwa uliomalizika kwa suluhu.


“Kweli Mkwasa amekabidhiwa gari, hii ni kama sehemu ya kumboreshea matakwa yake katika utendaji kazi. Sasa anatakiwa afike katika viwanja mbalimbali siyo tu kuishia kuangalia mechi za hapa (Dar) na tayari ameshakwenda Morogoro na atazunguka kwingineko,” alisema Lucas.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic