October 31, 2016


Kocha Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, amesema mpaka sasa hakuna mchezaji ambaye amejihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo, ndiyo maana staa wao Ibrahim Ajib amejikuta akipoteza nafasi mbele ya Mohammed Ibrahim ‘Cabaye’ kwenye michezo miwili mfululizo.

Ajibu, licha ya kuwa na uwezo mkubwa lakini alilazimika kukaa benchi kwenye mechi za Toto Africans na Mwadui ambazo hata hivyo kikosi hicho kiliibuka na ushindi na kujikita kileleni kwa kujikusanyia pointi 32.

Mayanja amesema kwamba lengo la kuweka suala hilo ni kutaka kuona kila mmoja anajituma kuhakikisha timu hiyo haina makundi kwa tabaka moja la wachezaji kujiona muhimu kuliko wenzao. 

“Kwetu hakuna mchezaji aliye staa kuliko mwenzake na hakuna mchezaji mwenye namba ndani ya kikosi cha kwanza kwani kila mmoja anaweza kukaa benchi na aliyekaa benchi akaanza, hiyo ni kulingana na mechi itakavyokuwa.

“Tunafanya hivyo kwa ajili ya kutotaka kuwafanya kundi la wachezaji fulani kujiona muhimu ndani ya timu lakini pia hata watakapokosekana tuwe na uhakika kwamba tunavuna pointi tatu bila ya wasiwasi wowote ule.

“Na siyo Ajibu peke yake ambaye amekutana na suala hili, bali tuna uwezo wa kumpumzisha yeyote yule na utaona ilimtokea Mavugo hivi karibuni na itaendelea kwa kila nafasi kwa ajili ya kuwafanya wachezaji kutobweteka na kuridhika kwani ikitokea hivyo basi tunaweza kupoteza ubingwa ambao tunausaka kwa kila hali,” alisema Mayanja.

Hata hivyo, kwa mtazamo wa kawaida kuna wachezaji ambao hadi sasa katika kikosi cha Simba wameishajihakikishia namba katika kikosi hicho.


Mfano mabeki Mohamed Zimbwe, Janvier Bukungu, Method Mwanjale, nahodha Jonas Mkude, viungo Muzamiru Yassin, kiungo Shiza Kichuya na kipa Vicent Agnban, hawa wanaonekana wamejihakikishia nafasi na wamekuwa wakiendelea kufanya vizuri ili kujihakikishia vizuri.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic