October 19, 2016



Wakati mkataba wake ukielekea ukingoni, beki kisiki wa Azam FC, Pascal Wawa, raia wa Ivory Coast, ameutahadharisha uongozi wa timu hiyo kwa kusema kuwa hahofii kitu chochote iwapo itatokea uongozi utakataa kumuongezea mkataba kwani ataenda kucheza sehemu yoyote.

Wawa alijiunga na Azam mwaka 2014 kwa mkataba wa mwaka mmoja katika usajili wa dirisha dogo akitokea El Merreikh ya Sudan kabla ya kuongeza mwaka mwingine ambao unatarajia kuisha hivi karibuni huku akiwa hajaichezea mchezo wowote msimu huu kutokana na kuandamwa na majeraha ya nyama za paja.

Wawa alisema kuwa hawezi kuhofia kitu chochote atakachoambiwa na uongozi wa timu hiyo kutokana na mkataba wake kufikia ukingoni kwa kuwa soka ndiyo kazi yake.

“Kiukweli kwa sasa nimeshapona kabisa na nafanya mazoezi yote na timu kila siku lakini suala la lini nitarejea uwanjani kucheza hilo ni jukumu la mwalimu ambaye anapanga nani anafaa kucheza kulingana na mchezo husika ila kwa upande wangu nipo fiti kwa asilimia zote kucheza michezo ya ligi.


“Lakini najua kwamba mkataba wangu unaelekea kumalizika ndani ya Azam na bado uongozi haujanieleza kitu chochote ila siwezi kuhofia hilo wala kujali kwa kuwa soka ndiyo maisha na kazi yangu, sasa lolote watakalosema wao nitakuwa tayari kulifuata kwa kuwa naamini bado sijachoka nitacheza sehemu yoyote,” alisema Wawa.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic