October 11, 2016


Ukiangalia haraka haraka unaweza kuona kama kila kitu kinakwenda kawaida kabisa. Lakini kikosi cha Yanga, kinakwenda kinapotea nafasi ya kubeba ubingwa.

Taratibu, Yanga inakwenda inapoteza mwelekeo kutokana na mgogoro ambao unaonekana kuzidi kuibana na kuubana uongozi wake.

Wanachama wa Yanga waliafikiana kwa pamoja kuikodisha timu na nembo yao kwa miaka 10 kwa kampuni ya Yanga Yetu Ltd.

Mchakato ukafanyika kwa zaidi ya mwezi mmoja na baada ya hapo kupitia wadhamini wakasaini mkataba huo ili ukodishwaji uanze.

Wakati hayo yakiwa yamekamilika, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) likaibuka na kusema halitambui na kutaka utaratibu ufuatwe kwa madai limepata malalamiko.

BMT ilikuwa imelala, wakati mchakato ukiendelea baada ya Wanayanga kukubali, kila kitu kilifanyika hadharani lakini hawakusimama na kusema.

Hao waliopeleka malalamiko, ilikuwa lini? Vipi BMT ilikaa kimya muda wote hadi isubiri mkataba usainiwe ndiyo iseme?

Lakini TFF ambayo pia ilikuwemo na imekaa kimya, imeibuka leo na kusema kama ilivyotamka BMT. Huenda TFF imeona sasa baada ya kusikia BMT imetamka.

Jiulize pia, TFF walikuwa wapi, vitu viliendelea na kama Yanga walikutana haikuwa halali, hawakusema lolote na ukimya wao ni ishara ya hakukuwa na tatizo.

Vipi TFF inasema sasa, haikusema kabla ya BMT kusema? Hapa utagundua kuna tatizo.

Mgogoro huu unaweza kuonekana kama ni mdogo, lakini kwa unavyokwenda hakuna ubishi unakwenda kuiangusha Yanga kama timu na mwisho inapunguza zaidi nafasi yake ya kuwa bingwa tena au kufanya vizuri.

Huenda wanaotaka Yanga kutoingia kwenye mabadiliko hayo kwa visingizio kibao, wakashindwa kwa kuwa wanachama wenyewe wa Yanga zaidi ya asilimia 95 wanataka nafasi hiyo ya mabadiliko.

Lakini hadi inafikia wamekubaliana au wamewashinda wanaotaka kuwazuia, tayari watakuwa wamepoteza nguvu ya usimamizi au mwendo kwenye Ligi Kuu Bara.

Kama wapinzani wao Simba au Azam FC wakiwa makini, basi Yanga wataisoma namba na watalazimika kusubiri mwakani ili mambo yaende sawa.

Kingine ambacho kinawaangusha Yanga, ni suala la wao wenyewe kujichanganya kutokana na taarifa kwamba wanataka kumuacha Kocha Hans Pluijm.

Kumekuwa na taarifa walizungumza na kocha Mzambia. Uongozi ulifanya kazi ya kukanusha, lakini bado haiwezi ikawa imesaidia sana wakati wana mchezo mgumu kesho dhidi ya Mtibwa Sugar.

Yanga wanalazimika kufanya kazi ya ziada kutenganisha timu na haya yanayotokea. Ingawa kuna ugumu lakini wachezaji wanatakiwa kujengwa kisaikolojia zaidi ili warejee katika mwendo sahihi.


6 COMMENTS:

  1. TFF ya MALINZI na BMT ya KIGANJA no majipu, ila kamwe hawatafanikiwa

    ReplyDelete
  2. Ujanja ujanja wa _manji_ 1.mmiliki Quality group. 2. Mwenyekiti Young africans football club. 3.Mmiliki Yanga yetu co. Ltd. 4.Quality group inaidai Young africans fc. Sh. 11700000000/-, zilizokopwa chini ya uonyekiti wake. 5.Yanga yetu co. Ltd., inaikodi timu ya mpira ya YAFC kwa kipindi cha miaka 10 kwa malipo ya Sh.Milioni 100 kwa mwaka. 6.Mwaka ambao Yanga yetu co.Ltd. watapata faida watailipa YAFC.asilimia 25 ya faida hiyo. 7.Wanachama wa YAFC. watamchagua mjumbe mmoja kuingia katika bodi ya Yanga yetu co.Ltd, pale tu idadi ya wanachama itakapofikia laki moja (100000). Leo wanachama wenye kadi ni chini ya 25000. 8.manji bado mwenyekiti wa YAFC. …TUJIULIZE… Mkataba huu una tofauti yoyote na ile ya Carl Peters na watemi wa zamani? ndio maana RC Makonda alisema "ukitaka kujua kwa nini nchi yetu ni maskini, wakati tuna raslimali kibao, basi utazame mkataba wa Manji na YANGA."

    ReplyDelete
  3. TFF na MBT wako sahihi salehe wasingeweza kusitisha wakati swala lilikuwa kwenye mchakato. Ili kuonyesha wewe ni kiongozi bora huwezi kufuatilia taaria ambazo si rasmi. Inabidi usubiri mpaka ziwe rasmi. na kuwa rasmi ndio hukusasa kwamba watu mamesha saini ndio unatakiwa kusitisha.

    kwa maana hiyo TFF na BMT wako sahihi kabisa na wameenda na muda muafaka. Huwezi kutukodishia timu kama Bodanoda bhana kwa ajili ya maslahi ya watu wachache.

    ReplyDelete
  4. Hivi Bakema1 Manji akijitoa ukiambiwa team haina hata nauli wewe utachanga? Acheni kuzingua wakati mnajua hamtoi hata senti tano na mnajua Yanga haiwezi tengeneza faida hata siku moja. Cha maana ni kungojea timu ishinde muwe na furaha tuu basi mambo ya uendeshaji hamuhusiki nayo..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Swali ni kwanin mkose nauli?...manji mpo nae tangu 1935?

      Delete
  5. Ni kukosa maarifa tu ndio kuna tusumbua...timu za simba na yanga ndio timu pekee zenye uwezo wa kujiendesha lakin kwa vile hatuna uaminifu, tume jaa tamaa ndio mana tuna fika hapa......wacha watusumbue kina manji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic