October 25, 2016



Kocha Charles Boniface Mkwasa yuko katika rada za Yanga na tayari wamefanya mazungumzo naye.

Mkwasa amezungumza na Yanga kuhusiana na suala la kurejea kuchukua nafasi ya kocha msaidizi.

Taarifa za ndani za Yanga, zinaeleza Mkwasa anaonekana kuwa mkali na anayetaka kufanya mambo yake kwa uahakika.

“Mkwasa ni mkali, kocha msaidizi anatakiwa kuwa ni yule ambaye hataki mchezo. Hivyo uongozi wa Yanga unaonekana kutaka kumrejesha.

“Umezungumza naye mara mbili na inawezekana kweli akarejea,” kilieleza chanzo.

Pamoja na Mkwasa, mwingine anayeweza kutua Yanga katika benchi jipya la ufundi ni Manyika Peter, kipa wa zamani wa timu hiyo ambaye amekuwa akifanya kazi na Mkwasa katika kikosi cha timu ya taifa.

Pia kiungo wa zamani wa timu hiyo, Sekilojo Chambua anapewa nafasi ya kuchukua nafasi ya meneje, Hafidhi Saleh.

Uamuzi wa Yanga unafuatia kubadilishwa kwa Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm na kumchukua George Lwandamina wakati Yanga ikiwa ndio imeanza kuamka.


1 COMMENTS:

  1. Kwa mawazo yangu Yanga wasingemshusha hivyo Mkwasa! Kama wana mwamini, nadhani umefika wakati wa kuwapa kipaumbele makocha wazawa. Mkwasa kaonyesha uwezo akiwa na kikosi cha T Stars. Wangempa kikosi kuliko kumrudisha ktk ukocha msaidizi. Jata kama ni mshahara utakao mtoa TFF (Stars) bado mimi naona nikumhaeirisha Mkwasa na kutomtakia maendeleo ki mataifa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic