November 5, 2016


Azam FC imeamua katika usajili wa dirisha dogo msimu huu kusajili washambuliaji watatu kwa gharama yoyote ile ili kukiweka sawa kikosi chao ambacho kipo nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Bara.

Makamu Mwenyekiti wa Azam, Idrissa Nassor ‘Father’, amesema vyovyote itakavyokuwa lazima wakiimarishe zaidi kikosi chao kwenye usajili wa dirisha dogo utakaoanza Novemba 15, mwaka huu.

Azam ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 22 ambapo kwenye mechi 13, imeshinda sita tu na kupoteza tatu ikiwa na sare nne, mwendo ambao Father anaamini siyo wa kawaida kwa timu yao.

Tayari Kocha Zeben Hernandez amewataarifu viongozi wa Azam kuhakikisha anaongezewa nguvu kwenye ushambuliaji ambapo Father amesema kuna sura mpya tatu za washambuliaji watakaosajiliwa.

“Washambuliaji wawili watatoka nje ya nchi na mmoja wa hapahapa nchini, tunataka kuhakikisha wanampa sapoti kubwa John Bocco katika kusaka ushindi,” alisema Father.

Father amesema kuwa katika kutekeleza hilo, watamleta fowadi wao Mghana Enock Ageyi ambaye anacheza Medeama kwa mkopo huku mikakati ya kusaka straika mwingine wa kimataifa ikirarajiwa kuanza muda wowote.

“Kweli mikakati ya kuboresha kikosi ipo na kwa kuanza kocha ameomba kuongezewa nguvu kwenye ushambuliaji. Mmoja tunataka awe mzawa na mwingine wa kimataifa ambaye ataungana na Ageyi ambaye tulimuacha kwa mkopo Medeama, naye anakuja ili kujaribu kumuongezea nguvu Bocco,” alisema Father.

“Kwa ujio wa Ageyi tutakuwa na wachezaji wa kigeni zaidi ya kanuni, hivyo lazima tumuache au tuwaache wengine ili kupisha hao wapya.”


Waivory Coast, beki kisiki, Pascal Wawa na Frasciso Zukumbariwa huenda safari ikawakuta kutokana na mchango wao mdogo katika timu kwani Wawa hajacheza mechi yoyote msimu huu ikidaiwa haelewani na Zeben.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic