November 23, 2016


Uongozi wa Yanga juzi Jumatatu kupitia kwa Makamu wake Mwenyekiti Clement Sanga ulitangaza kuwa licha ya mabadiliko uliyoyafanya katika benchi lake la ufundi, aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm haondoki  popote ila atakuwa mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo na nafasi yake itachukuliwa na Mzambia, George Lwandamina.

Kutokana na hali hiyo, mshambuliaji wa kutumainiwa wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe amedai kuwa kitendo cha Pluijm kuamua kubaki klabuni hapo na kusaidiana kazi na Lwandamina amekipokea kwa mikono miwili, hivyo wapinzani wao watakoma.

Uongozi wa Yanga ulifikia uamuzi huo wa kufanya mabadiliko hayo kwa lengo la  kuliongezea nguvu benchi lake la ufundi ili kuhakikisha timu hiyo inatetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Bara lakini pia iweze kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itashiriki hapo mwakani.

Tambwe amesema kuwa muunganiko wa makocha hao wawili katika benchi la ufundi la timu hiyo, utaleta mapinduzi makubwa ndani ya timu katika kipindi hiki ambacho inapambana kuhakikisha inatetea ubingwa wa ligi kuu.

“Baada ya kuzipata taarifa hizo nimefurahi sana kwa sababu wote wawili ni makocha wakubwa hapa Afrika, hivyo muunganiko wao utaleta mapinduzi makubwa katika kikosi chetu.

“Lakini pia hali hiyo itaongeza morali kwa sisi wachezaji katika harakati zetu za kuhakikisha tunapambana vilivyo kutimiza malengo yetu tuliyojiwekea msimu huu, ukiachana na ubingwa wa ligi kuu lakini pia kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa,” alisema Tambwe ambaye kwa sasa yupo kwao Burundi kwa mapumziko ambayo wachezaji wote wa timu hiyo walipewa baada kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic