November 26, 2016



Kocha wa Simba, Joseph Omog mjanja sana kwani amewaambia viongozi wa Simba ana nafasi tatu za wachezaji ambao anataka wamuongezee nguvu kikosini.

Mmoja wa mabosi wa Kamati ya Utendaji ya Simba ambayo ndiyo ya kwanza kuona ripoti ya kocha, amesema kwamba, anataka wamsajilie kipa, beki na straika mmoja.

Katika ripoti yake, Omog ametoa sifa tu za wachezaji anaowataka huku akiacha zoezi la kuwasajili kwa viongozi lakini akasisitiza hahitaji straika kutoka nje ya nchi kwani atapata presha kama ilivyo kwa waliopo.

Simba ina mastraika Laudit Mavugo raia wa Burundi na Fredrick Blagnon wa Ivory Coast ambao bado hawajaonyesha uwezo mkubwa katika Ligi Kuu Bara katika mechi 15 za Simba.

Kabla ya kuiona ripoti ya Omog, baadhi ya viongozi wa Simba ambao wameona Mavugo na Blagnon walivyochemsha, wakaanza mipango ya kumrejesha kikosini Emmanuel Okwi kutoka SønderjyskE ya Denmark.

“Kutokana na ripoti ya Omog, sasa hatuna tena mpango wa kumsajili Okwi kwani itakuwa kinyume na matakwa ya kocha hivyo tunaendelea na mambo mengine kwa kufuata anachotaka yeye (Omog).

“Tulidhani Okwi akija atafanya vizuri moja kwa moja kwani anaijua ligi yetu, lakini kocha ameshikilia msimamo wake wa kutaka straika kutoka ndani ya nchi, hatuna jinsi tunafuata kile alichosema,” alisema bosi huyo.


Licha ya viongozi wake kutokuwa tayari kuweka wazi kuhusu usajili wa straika mzawa, gazeti hili linafahamu Simba inamfukuzia Victor Hangaya wa Prisons ili iweze kumsajili.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic