November 25, 2016


Baada ya kutambulishwa rasmi, Kocha mpya wa Yanga, George Lwandamina amesema atapambana vilivyo kuhakikisha anafanya vema.

Lakini Lwandamina raia wa Zambia, amekiri kuwa kweli ni jukumu gumu kwake kama changamoto.

“Lakini nitapambana kufanya vizuri, najua ni changamoto mpya kwangu lakini nitafanya kila linalowezekana,” alisema.

Lwandamina ambaye kwa mara ya kwanza alifanya mahojiano na SALEHJEMBE ameomba Wanayanga kumpa ushirikiano ili kufikia malengo yake.

Awali aliwahi kuiambia SALEHJEMBE kwamba anapenda soka la kushambulia pia kukaba pamoja. Lakini akasisitiza suala la ushrikiano ni namba moja kwake.


Leo ametambulishwa kwa waandishi wa habari akiwa pamoja na Hans van der Pluijm.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic