November 6, 2016





MPIRA UMEKWISHAAA
-GOOOOOOOOOOOO Lyon wanapata bao kabisa baada ya mfungaji kupokea krosi, lakini mpira unagusa mkono na yeye hafanyi ajizi anapachika ba
-SUB Lyon wanamtoa Omary Abdallah anatoka anaingia Raidhan Hafidhi
-Basi la Lyon linaonekana halina hata njia ya kupita, Simba wanashambulia kwelikweli, lakini hakuna nafasi

DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Dk 89, Lyon wanaonekana kupoteza muda zaidi ili kuhakikisha wanapata pointi moja leo
Dk 83, mechi bado ngumu kwa kila upande ingawa Simba wanafanya mashambulizi mfululizo kuhakikisha wanaitoboa ngome ya Lyon
Dk 81, Simba wanapata kona baada ya Isihaka kuutoa mpira, inapigwa wanaokoa, kona nyingine, kinapigwa kichwa safi lakini anawahi
Dk 80, krosi ya Kichuya, Mavugo anaruka na kuunganisha, kipa anadaka kwa ulaini, anaanguka chini kupoteza muda
Dk 75, Kichuya anapiga mpira mkali wa adhabu inakuwa kona., Inachongwa vizuri hapa, goal kick

Dk 72, Simba wanafanya shambulizi jingine kali, lakini Muzamiru anabutua pembeni kabisa
Dk 67 sasa, wanachofanya Lyon ni kuupoza mpira na kucheza taratibu kabisa. Inaonekana wanachotaka cha kwanza ni sare, ushindi kama itatokea kwao pia itakuwa poa
Dk 62, kipa Lyon anadaka mpira lakini anaonekana kuwa anapoteza muda kwa makusudi
Dk 59, Miraji Adam anaokoa mpira miguuni mwa Mavugo, ilikuwa krosi safi ya Kichuya

Dk 57, milango bado migumu sana, Lyon wanachofanya, wengi wamerudi nyuma na wanafanya mashambulizi ya kushitukiza
Dk 51, pasi nzuri ya Kichuya, Mwanjale anaachia shuti kali hapa lakini ni goal kick
SUB DK 50, Mo Ibrahim anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Ibrahim Ajibu
Dk 49, shambulizi kali hapa kwenye lango la Lyon, mpira unagonga mwamba na kuokolewa
Dk 46, mpira umeanza lakini taratibu saaaana kwa kila upande kama ni watu wanaosomana hivi.

MAPUMZIKO

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 44, Mavugo anapiga mpira mzuri ndani ya lango la Lyon lakini kipa anakuwa mwepesi kuwahi
Dk 39, Miraji Adam anaachia free kick, hatari, mpira unagonga mwamba au mtambaa wa panya na Simba wanaokoa
KADI Dk 37, Bukungu analambwa kadi ya njano kwa kucheza faulo nje kidogo ya eneo la 18 la Simba, anakwenda kupiga miraji Adam ambaye ni hatari kweli kwa mipira hiyo
Dk 34, nje ya 18, Mwanajale anajaribu kuachia shuti lakini anapiga juuuuu
Dk 31, Kona wanapata kona ya pili baada ya Isihaka kujichanganya na kipa wake, inachongwa lakini goal kick
Dk 24, Simba wanaingia vizuri, Mavugo anatoa pasi nzuri kwa Mavugo. Anaachia shuti kali hapa lakini Isihaka Hassan anaokoa na kuwa kona ya kwanza katika mechi hii na kona ya kwanza ya Simba. Inachongwa, Lyon wanaokoa

Dk 19, tokea nyuma Mwanjale anapanda akitoa na kupewa, anatoa anarudishiwa hadi amefikia kupiga shuti kwenye lango la Lyon lakini kipa anadaka vizuri kabisa
Dk 16, Simba wanagongeana vizuri, Kazimoto anatoa pasi safi kwa Mo Ibrahim lakini mwamuzi anasema ni offside
Dk 15, Simba wanaingia vizuri tena lakini Kichuya anapiga shuti kuuubwaaaa
Dk 3 hadi 8, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja na Simba ndiyo wamefika mara tatu kwenye lango la Lyon lakini hakuna mashambulizi makuwa
DK 1, mechi imeanza kwa kasi na Simba wanasifika kwenye lango la Lyon ambao wanaonekana wako makini. Sasa zaidi mpira unapigwa katikati ya uwanja


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic