November 5, 2016



Kuna uwezekano mkubwa, Kocha Mkuu wa Zesco raia wa Zambia, George Lwandamina akatua nchini leo Jumamosi kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuifundisha Yanga, lakini hiyo itategemea na hali ya mtoto wake.

Mzambia huyo, alitua nchini wiki moja iliyopita kwa ajili ya kufanya mazungumzo na timu hiyo ili aje kuchukua nafasi ya Mholanzi, Hans Pluijm.

Lwandamina amezungumza na SALEHJEMBE moja kwa moja kutoka Lusaka, Zambia na kusema inawezekana ikawa hivyo, ikishindikana inaweza kuwa kesho.

“Ninaweza kuja Tanzania kesho (leo) kama mambo yakienda vizuri kwani mtoto wangu ni mgonjwa hivyo kuna watu wameenda kunitazamia tiketi ili niweze kuja Tanzania,” alisema Lwandamina alipozungumza na gazeti hili kutoka Zambia.

"Kama itashindikana, huenda ikawa Jumapili au Jumatatu, lakini nitakuja," alisema Lwandamina.

Kocha alisema awali alishindwa kusaini mkataba huo kutokana na kubanwa na mkataba wa Zesco unaotarajiwa kumalizika Januari, 2017.

Kama kusaini mkataba, Lwandamina angesaini tangu kipindi kile alivyokuja nchini kufanya mazungumzo na Yanga, lakini ikashindikana kutokana na kubanwa na mkataba wake.

Taarifa kutoka Zambia zinasema kocha huyo tayari amemalizana na viongozi wa Zesco na leo atatua nchini kwa ajili ya kusaini mkataba na Yanga.


Yanga bado inafanya siri ujio wa Lwandamina na hata tukio hilo la kusaini mkataba kwani bado inaye Kocha Hans van Der Pluijm ambaye alikataliwa kujiuzulu na uongozi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic