November 15, 2016

MANARA


Na Haji Sunday Manara aliyekuwa Harare
Ninashudia aibu nyingine katika nchi za watu kwa kichapo kizito kutoka kwa Zimbabwe kwenye Uwanja wa Taifa wa Harare. Ni kipigo tulichokiandaa sisi wenyewe na ingakuwa ni miujiza walau kupata sare kule kwa Washona na Wandebele.

Wazimbabwe huku wakijua wanajiandaa na Afcon mapema mwakani walileta mziki kamili wa professionals wao karibia wote, huku akina sisi tukiwa na pro wetu wawili Mbwana Samata na Elius Maguli wa FC Dhoufar ya kule Salala nchini Oman. Pia Ulimwengu akiwa nje.
Wakati sisi tulikuwa na pro hao wenzetu wachezaji wanaocheza ligi ya kwao iliyobakisha mechi mbili ni wawili tu...
Yaani hapo ni kinyume nyume na usisahau pro waliowaleta wanatamba huko ughaibuni kuanzia Belgium, Holland, Sweeden, Denmark hadi wale nyota wao wanaokipiga Keizer Chief na Mamelodi Sundowns ambao ndiyo mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sasa. 
Nimesoma baadhi ya maandishi ya watanzania wenzangu baada ya kichapo cha Harare na kushangazwa kidogo.
Eti Mkwasa uwezo wake umeishia hapa, uuh lalaaa!! Hizi lugha zimeanza kutawala sana siku hizi katika soka, naiona siku yangu ntakayoambiwa na washabiki wetu kuwa uwezo wangu katika usemaji wa klabu utakaposemwa umeishia hapa. Kisa labda timu imefungwa na Orlando Pirates.   Kwangu hizi ni lugha za hovyohovyo zinazoakisi uwezo wetu duni wa kupambanua mambo, nini kosa la Mkwasa katika hili?? 

Unategemea nn baada ya kuwakusanya wachezaji waliochoka na safari za ligi kuu inayobadilishwa ratiba kila uchwao!! 

Tunapojadili vitu tupendelee kuangalia uhalisia, eti kanuni zinaruhusu klabu kupeleka wachezaji siku moja kabla kwa mechi za kirafiki huko.

Ni ujuha kufikiri tu kuwa hawa local players wetu wapo tayari kupambana na pro wa aina ya Musona wa Zimbabwe na wenzie. Yaampasa kocha walau apate siku tano angalau atrain na wachezaji wake, 
Sikuona kwa nn ligi haikusimama wiki iliopita ili kumpa fursa kocha kidogo, nini kinalazimisha ratiba yetu kuwa na mbanano huu?!! Katika hili, Bodi ya Ligi nayo ijipime upya.

Tuelewe hizi kanuni za FIFA ziliwalenga wachezaji na nchi za kiweledi, kwetu hazitatusaidia na lazma bodi na TFF wazingatie uwezo wa wachezaji wetu na ligi yenye.

Ligi nyepesi yenye ushindani duni na maamuzi mabovu sambamba na tuhuma chungu mbovu..

Ligi inayotumia malando badala ya viwanja halisi vya ndiki, kisha makocha wa mitandaoni wanamlaumu Mkwasa. 
Kocha mweledi na mwenye historia safi katika medani ya futboli nchini, humfungi mtu ndugu mbongo kwa pro wawili au watatu labda utamuotea Somalia na Djibout, kwa sasa ukiingia hata na Comoro inabidi ubane ashua zako.

Wenzetu Zimbabwe wana kitengo maalum katika shirikisho lao kuhakikisha kinapeleka pro wengi nje. Sisi tunapiga porojo tu. 
Zimbabwe yenye uchumi wa hovyo lakini hakuna tuhuma za hovyo hovyo. Wao hapa Dar ni kama Dubai kwa wafanyabiashara wao. lakini uwanjani kwetu sisi ni kama wanacheza na watoto wa shule, kama yule abiria aliyemuuliza Samata nyie ni timu ya chuo?? 
Hatuwezi kupiga hatua kama hatuwekezi kupata pro wengi, never on earth. 
Iangalie Uganda leo ina pro wangapi?   wajisemee waunguja, ndio baaaasi tena, washatuacha!!! 
Ahhh nisiseme sana, his ni nchi yangu na sina taifa lingine lolote. bt tuiunge mkono kila jitihada za kunusuru mpira toka TFF na vilabu vyetu na tusijtie kila mmoja kocha au mjuaji,
Vinginevyo Somalia wakimaliza vita watakuja kutufunga hapahapa.

2 COMMENTS:

  1. Umeishia kulaumu badala ya kueleza nini kifanyike!! Mapro hawapelekwi bali wanatengenezwa!! Samata alipelekwa na nani!?

    ReplyDelete
  2. manara leo umeongea hoja nzuri sana umeacha mbali itikadi na mapenzi yako kitimu.
    ni wazi na ukweli kuwa kipigo hicho tulikiandaaa wenyewe, unawezaje kuwatoa wachezaji waliotoka kwenye michezo ya kuifia timu eti ndo wakacheze na watu waliopumzika muda wa kutosha na kujinoa na mecchi hiyo? kama yanga ilikuwa ikicheza alhamisi na ilikuwa kila mchezaji aliyeitwa taifa stars ni muhimu pia katika kubadili kupata matokeo ya mchezo huo wa kumalizia mzunguko wa kwanza, ijumaa asafsiri jumamosi apumzike na jumapili awe uwanjani kusaka point 3 kwa waliojipanga!!!
    ni ajabu katika sooka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic