November 4, 2016



Pamoja na kuifunga Yanga mabao 2-1, Kocha wa Mbeya City, Kinnah Phiri, amesisitiza kuwa Yanga inacheza soka hatari zaidi kulinganisha na vinara wa ligi, Simba ama Azam ambazo tayari amekutana nazo na zikachomoza na ushindi dhidi yao.

Phiri aliiongoza Mbeya kupata ushindi huo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa mabao ya Hassan Mwasapili na Kenny Ally huku Donald Ngoma akiifungia bao pekee Yanga, wakati awali Azam iliichapa mabao 2-1 kabla ya Simba kushinda mabao 2-0 uwanjani hapo.

Pamoja na kufungwa na Azam na Simba lakini Phiri anasema kiufundi, Yanga bado ndiyo timu iliyozingua kati ya hizo na kusisitiza kama siyo kuwahimiza vijana wake kabla ya mchezo, wangekula nyingi kutokana na mfumo wao wa mashambulizi ya kulazimisha.

PHIRI

“Bado Yanga ndiyo timu hatari kati ya hizo. Naamini kwa soka walilocheza dhidi ya Yanga, tungecheza vile dhidi ya Simba ama Azam uhakika wa ushindi ungekuwepo, lakini wengi walikuwa na woga mwingi na kujikuta tunafungwa.

“Lakini dhidi ya Yanga niliwahimiza kujiamini, wasiangalie majina ama ubora wa timu, badala yake wacheze kitimu zaidi na kweli tukafanikiwa, lakini ukweli ni kwamba Yanga ilitupa presha sana, sanasana kipindi cha pili, (Simon) Msuva alikuwa mtu hatari zaidi,” alisema kocha huyo wa zamani wa Free States ya Afrika Kusini.


2 COMMENTS:

  1. Ni kawaida mtu kumpa moyo mnyonge wake kuliko kumkubali m'babe wake. Siku ya simba alisema beki alishondwa kumzuia Kichuya. Piga siasa tu Phiri, Simba hatutakagi sifa.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic