November 9, 2016





FULL TIME

Mwamuzi anamaliza mchezo, Tanzania Prisons wanaibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba.
 
Dakika ya 90 + 7: Mchezo unaweza kumalizika muda wowote kuanzia sasa, matokeo bado ni 2-1.
 
Dakika ya 90 + 2: Simba wanapata kona, anapiga Kichuya lakini unaokolewa na walinzi wa Prisons.



Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaongeza dakika 5 za nyongeza.



Dakika ya 81: Mavugo na Kichuya wanafanya shambulizi la kushtukiza lakini mabeki wa Prisons wanawahi na kuokoa.

Dakika ya 76: Mchezo unaendelea.

Dakika ya 75: Hangaya yupo chini, anatolewa kwa machela baada ya kuumia alipogongana na Lufunga wa Simba. 
 
Dakika ya 68: Simba wanamtoa Mwinyi Kazimoto anaingia Ibrahim Mohamed.

Dakika ya 66: Mchezaji wa Prisons, Jumanne Elfadhili anapewa kadi ya njano kwa kuchelewesha muda.
 
Dakika ya 63: Prisons wanapata bao la pili, mfungaji ni yuleyule Hangaya, anafunga kwa kichwa na kwa staili ileile. Ilipigwa mpira wa pembeni mabeki wa Simba wakafanya uzembe, akaruka juu na kufunga.
 
GOOOOOOOOOOOOOO!!!
 
Dakika ya 61: Simba wanaongeza kasi lakini Prisons, nao wanaonekana kuwa vizuri.
 
Dakika ya 55: Hangaya anafanya shambulizi, anapiga shuti lakini linapaa juu la lango la Simba.
 
Dakika 50: Prisons 1, Simba 1, mchezo unaendelea kwa kasi.
 
Dakika ya  48: Prisons wanapata bao la kusawazisha mfungaji akiwa ni Victor Hangaya, amefunga baada ya kuunganisha mpira wa krosi ya Kimenya.

Dakika ya 47: GOOOOOOOOOO!!!!
 
Dakika ya 46: Kipindi cha pili kimeanza.
 
HALF TIME:

Mwamuzi anapuliza kipenga kukamilisha kipindi cha kwanza cha mchezo huu. Timu zote zinaelekea vyumbani kupumzika.

Dakika ya 45: Simba wanafanya shambulizi lakini mpira unatoka nje.

Dakika ya 43: Simba wanapata bao la kwanza, mfungaji ni Jamal Mnyate, anafunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Shiza Kichuya 

GOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!

Dakika ya 40: Salum Kimenya anafanya shambulizi kali lakini mpira unatoka nje.

Dakika ya 36: Prisons wanapata kona, inapigwa lakini inaokolewa na walinzi wa Simba.
 
Dakika ya 35: Prisons wanaonekana kujipanga na kufanya mashambulizi.
 
Dakika ya 28: Simba wanapata faulo nje ya eneo la 18 ya Prisons, Mwanjale anapiga suti lakini kipa Ntalla analiona na kulidaka.
 
Dakika ya 22: Prisons wanapata kona, wanapiga inababatiza walinzi wa Simba na inakaribia kuingia wavuni lakini mpira unatoka nje na kuwa goal kick.

Dakika 15: Prisons wanajibu shambulizi kwenye lango la Simba lakini inaokolewa na walinzi wa Simba.
 
Dakika ya 12: Simba wanafanya shambulizi kali, Mavugo anashindwa kutumia vizuri nafasi aliyopata.
 
Dakika 9: Prisons wanafika kwenye lango la Simba lakini kipa Agban anauwahi mpira na kuudaka.

Dakika ya 4: Mchezo unaanza kuongezeka kasi taratibu, bado timu zinasomana.

Dakika ya 1: Mchezo umeanza hapa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
 
Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kuanza muda wowote hapa kwenye Uwanja wa Sokine kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Simba.

KIKOSI CHA SIMBA HIKI HAPA:
1.Agban Vicent, 2 . Hamad Juma. 3.Mohamed Hussen, 4.Novaty Lufunga, 5 . method Mwanjali, 6 . Jonas Mkude, 7.Shiza Kichuya, 8.Mzamiru Yasssin, 9.Laudit Mavugo, 10.Mwinyi Kazimoto, 11.Jamal Mnyate.

Sub:
Peter Manyika, Emmanuel Simwanza, Said Hamis, Mohamed Ibrahim, Ndusha Mussa, Haji Ugando

KIKOSI CHA TANZANIA PRISONS
1. Andrew Ntala, 2. Salum Kimenya 3. Leonsi Mutalemwa, 4 . Jumanne Elfadhili 5. James Mwasote 6 . Kazungu Mashauri, 7. Lambarti Sabiyanka, 8. Mohamed Sammata 9. Victor Hangaya, 10. Salum Bosco 11.Benjamin Asukile

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic