November 16, 2016

OMOG

Unaweza kusema kila mbuyu na shetani wake aisee! Kocha wa Simba, Joseph Omog pamoja na kufungwa mechi mbili mfululizo za mwisho dhidi ya African Lyon na Prisons huku ikiponea chupuchupu kwa Yanga, bado humwambii chochote mbele ya Stand United.

Simba imekwenda likizo ikiwa ndiyo timu iliyochota pointi nyingi zaidi, ikiwa kileleni na pointi 35, mbili zaidi ya Yanga iliyo nafasi ya pili, lakini bado haamini Yanga kuwapumulia kisogoni ni sababu ya kuiita timu bora kiufundi, kwani kwake Stand ndiyo ilikuwa timu ngumu kiufundi kati ya timu 15 alizokutana nazo.

Akitoa tathmini yake ya raundi ya kwanza, Mcameroon huyo wa zamani wa Azam, alisisitiza licha ya kupoteza mbele ya Prisons na awali African Lyon, lakini Stand ndiyo timu atakayoikumbuka kwenye raundi ya kwanza.

“Bahati mbaya kila mchezo ulikuwa kama fainali kwetu, kadiri mechi zilivyokwenda lakini niwe mkweli, Stand ndiyo ilitupa shida sana. Ndiyo ilikuwa ngumu japokuwa tulishinda (bao 1-0) lakini ndiyo timu ninayokwambia ilitusumbua sana, japo timu nyingine zilitusumbua pia.

“Yanga inakuja katika nafasi ya pili, Azam inafuatia na nyingine zitafuata baada ya hizo timu. Kwangu hizi ndizo zilikuwa na ushindani mkubwa kuliko,” alisema Mcameroon huyo.

Katika mechi 15, Simba ilifanikiwa kushinda mechi 11, sare mbili huku ikipoteza michezo miwili dhidi ya Lyon na Prisons.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic