November 8, 2016

RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI

Kuonyesha kweli Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) haliko makini, ni baada ya kuipangia mechi ya Yanga dhidi ya JKT Ruvu kuchezwa kesho Jumatano, halafu ndani ya saa tatu, likaahirisha tena na kutoa taarifa itachezwa keshokutwa Alhamisi.

Mechi hiyo ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ilikuwa kiporo, TFF ikaipangia kuchezwa Jumatano na ikatoa taarifa kwa vyombo vya habari saa 9:31 Alasiri.

Lakini ilipofika Saa 12:33 ikiwa ni saa 3 na dakika 3, TFF ikatangaza kwamba mechi hiyo sasa itachezwa Alhamisi.

Hii ilikuwa ni baada ya JKT inayomilikiwa na Jeshi, kutia mkwara na kusema haitacheza mechi hiyo na TFF ikagundua iliboronga na kuufyata. 

Soma taarifa zote...

TAARIFA YA LEO SAA 12:33 JIONI
Wakati michezo miwili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikifanyika kesho Jumatano Novemba 9, 2016, mchezo kati ya Young Africans na Ruvu Shooting utafanyika Alhamisi Novemba 10, 2016 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, imefahamika.
Mchezo huo umesogezwa mbele kwa siku moja kwa sababu Ruvu Shooting imechelewa kutoka Bukoba mkoani Kagera ambako Jumapili iliyopita ilicheza na Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limejiridhisha kuwa Ruvu Shooting imechelewa kuingia kituo cha Dar es Salaam, ndiyo maana mchezo dhidi ya Young Africans umesogezwa mbele.
Michezo mingine ya kesho Jumatano inahusisha timu za Mwadui ya Shinyanga na Azam FC ambayo ilipewa jina la Mechi Na. 57 itachezwa Uwanja wa Mwadui wakati Simba itasafiri hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons katika mchezon Na. 60 Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.
Mechi zilipangiwa ratiba, lakini tarehe zake hazikupangwa (TBA). Tayari Bodi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imewasiliana na wahusika kuhusu mabadiliko hayo.
Sababu ya kuvuta nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya maandalizi ya kambi ya timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri Ijumaa wiki hii kwenda Harare Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika Novemba 13, maka huu.

TAARIFA YA LEO SAA 9:31 ALASIRI
Zile mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara za raundi ya Nane Duru la Kwanza, sasa zitafanyika kesho Jumatano Novemba 9, 2016.

Michezo hiyo inahusisha timu za Mwadui ya Shinyanga na Azam FC ambayo ilipewa jina la Mechi Na. 57 itachezwa Uwanja wa Mwadui wakati Simba itasafiri hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons katika mchezon Na. 60 Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.

Mchezo mwingine utazitanisha Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Uhuru jijini katika mchezo Na.59.

Mechi zilipangiwa ratiba, lakini tarehe zake hazikupangwa (TBA). Tayari Bodi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imewasiliana na wahusika kuhusu mabadiliko hayo.


Sababu ya kuvuta nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya maandalizi ya kambi ya timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri Ijumaa wiki hii kwenda Harare Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika Novemba 13, maka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic