November 24, 2016




Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limecharuka na kuitaka Simba kuonyesha heshima kwa kufuata utaratibu.

Kauli hiyo ya TFF inafuatia ile kauli ya Simba ya kusisitiza inataka waamuzi kutoka nje ya nchi na kama TFF isipofanya hivyo, watakapokutana na watani wao wa jadi Yanga, hawatapeleka timu uwanjani.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas Mapunda amesema wao wataendelea kuwatumia waamuzi wa Tanzania na kama Simba hawatapeleka timu, wao wanasubiri.

“Vizuri tukaheshimiana, watu wafuate taratibu na wajue waamuzi ndiyo wanaowachezesha mechi zao,” alisema.

“Sidhani kama ni sahihi kuanza kupangua waamuzi wa nyumbani kwa kuwa tu watu fulani hawataki. Kama wao hawatapeleka timu, sawa. Unawadharau unapokutana na Yanga, lakini haohao wanachezesha mechi yako dhidi ya timu nyingine kama JKT, Ndanda.”

Msemaji wa Simba, Haji Manara, juzi alisema wao hawatapeleka timu hadi TFF itakapotumia waamuzi kutoka nje ya Tanzania.


Manara alilalama kwamba waamuzi wamekuwa hawachezeshi kwa haki hasa Simba inapokutana na Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic