November 21, 2016



Pamoja na kufanya vema raundi ya kwanza, lakini ndani ya kikosi cha Stand United hali imezidi kuwa tete, hii ni baada ya shinikizo la zaidi ya milioni 124 wachezaji wanazoidai timu hiyo huku hatima ikiwa haijulikani.

Stand ilijizatiti kucheza mechi 10 mfululizo bila kupoteza na kumaliza mzunguko wa kwanza ikiwa katika nafasi ya sita, hata hivyo uongozi umeingiwa na hofu ya kuboronga raundi ya pili kutokana na wachezaji kuwakaba koo kutaka fedha za usajili huku baadhi yao wakiwa wameshanza migomo.

Katibu wa Stand, Kennedy Nyangi amelithibitishia Championi Jumatatu kudaiwa kiasi hicho, kikiwa ni majumuisho ya fedha za usajili na kuinyoshea kidole Kampuni ya Acacia kuwa ndiyo yenye jukumu hilo.

“Kweli tunadaiwa na niwe mkweli hakuna mchezaji hata mmoja aliyelipwa fedha ya usajili mpaka kwa wale waliosajiliwa msimu huu. Lakini yote yanakwamishwa na wadhamini wetu, Acacia ambao katika mkataba wa udhamini walibainisha kuwa ndiyo watakuwa na jukumu la kulipa fedha za usajili na sisi tutalipa mishahara tu,” alisema Nyangi na kuendelea:

“Lakini hawajatimiza hilo na tulitaka tuchukue hatua zaidi ila mbunge Stephen Masele (Jimbo la Shinyanga Mjini) alitutaka kusubiri, atakutana na uongozi wa Acacia kutaka kutafuta suluhu.

“Iwapo mambo yatakwenda hivi, kuna hatari kubwa raundi ya pili kwani baadhi ya wachezaji wameanza kugoma wakitaka walipwe kwanza fedha."

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic