November 30, 2016


Kutokana na kutokuwepo nchini kwa Kocha Mkuu wa Azam, Zeben Hernandez, dili la klabu hiyo kumsajili kiungo wa Mbeya City, Joseph Mahundi limekwama mpaka atakaporejea kocha huyo kutoka Hispania.

Mahundi ambaye alikuwa akifukuziwa kwa muda mrefu na Azam kwenda kusaidia safu ya kiungo mshambuliaji, atajiunga na Azam akiwa huru baada ya mkataba wake na Mbeya City kumalizika.

Meneja wa mchezaji huyo, Herry Chibakasa ‘Mzozo’, amesema tayari wameshafanya mazungumzo ya awali, lakini kinachochelewesha dili hilo ni kutokuwepo kwa kocha huyo mkuu ambapo Azam imesema haitaki kufanya usajili bila ya uwepo wake.

“Kila kitu kinaenda sawa, tayari tushafanya mazungumzo ya awali na yameenda vizuri, mchezaji wangu huyu yupo huru kutokana na mkataba wake kumalizika, hivyo naamini hakuna kipingamizi cha yeye kushindwa kujiunga na Azam kama taratibu zikifuatwa.

“Mpaka sasa ishu haijakamilika kutokana na kwamba makocha wao hawapo hasa mkuu kwani Azam wanataka usajili unapofanyika na wao wawepo, hivyo wamesema anarudi Desemba 2, ndiyo tutamaliza dili hilo,” alisema Mzozo.

Mpaka sasa Azam imeshakamilisha usajili wa wachezaji watatu wa kigeni ambao ni Enock Atta Agyei, Samuel Afful na Yahaya Mohammed wote kutoka Ghana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic