November 16, 2016


Kocha Mkuu wa Azam FC, Mhispania, Zeben Hernandez, amesema kuwa amevutiwa na uwezo unaoonyesha na wachezaji waliofanya majaribio kwenye timu hiyo wakiwemo wachezaji wa Medeama wa Ghana, kiungo Enock Atta Agyei na  mshambuliaji Benard Offori.

Azam juzi Jumatatu ilicheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi huku wachezaji hao wakionyesha uwezo mkubwa kwa kusaidia timu yao kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Hata hivyo, Agyei tayari ameshamalizana na uongozi wa timu hiyo baada ya kuingia mkataba wa miaka mitatu huku Offori na wengine wakisubiria ripoti ambayo mwalimu anayotarajia kuikabidhi kwa uongozi wakati wowote.

Zeben amesema kuwa amefurahishwa na uwezo unaoonyeshwa na wachezaji hao huku akiwa na imani ya kufanya vizuri zaidi katika mzunguko wa pili kutokana na ubora wa wachezaji hao.

“Wakati tunaanza ligi hatukuwa katika wakati mzuri kwa sababu tulikuwa na majeruhi wengi halafu timu haikuwa na washambuliaji wazuri ambao wangeweza kutusaidia kufikia malengo ambayo tunayatarajia.


“Lakini nadhani sasa kila kitu kitakuwa sawa kwa sababu tuna wachezaji wengi ambao wanafanya majaribio na kila mmoja amekuwa akionyesha kujituma, hilo linanipa hamasa ya kuweza kufanya vizuri ikiwezekana kuchukua ubingwa kwani wote wanaonyesha uwezo mkubwa,” alisema Zeben.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic