December 11, 2016


Kocha wa Yanga, George Lwandamina amesema namna walivyocheza katika mechi ya JKU ambayo wamelala kwa mabao 2-0, ni jambo zuri kwake.

Lwandamina raia wa Zambia amesema kikubwa alichotaka katika mchezo huo ni kuona kikosi chake.

“Hii ni mechi ya kwanza, ningeshinda ni jambo zuri kwa rekodi. Lakini kwanza nilitaka kuona timu hasa wachezaji.

“Mazoezini na kwenye mechi tofauti, hivyo pale unaweza kumuona mchezaji vizuri kabisa,” alisema.

Yanga ililala kwa mabao hayo 2-0 katika mechi hiyo ya kirafiki, jana huku Lwandamina akianza mechi na kikosi cha wale wachezaji ambao hukaa benchi au wanaopata nafasi ndogo ya kucheza.

Kipindi cha pili alifanya mabadiliko ya kikosi kizima kwa asilimia 90.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic