December 7, 2016



Kikosi cha Simba kitacheza mechi yake ya kwanza ya kirafiki ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa pili, Jumatatu.

Msemaji wa Simba, Haji Sunday Manara amesema kikosi chao kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Power Dinamo ya Zambia.

"Mechi hiyo itachezwa Jumatatu ya Desemba 12 kwenye Uwanja wa Uhuru, hii ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili," alisema Manara.

Tayari Simba ambao wamemaliza mzunguko wa kwanza wakiwa kileleni, wako kambini mjini Morogoro wakifanya maandalizi.

Dynamo ilianzishwa mwaka 1971, imewahi kubeba ubingwa wa Zambia mara 6 na mara ya mwisho ikiwa ni 2011, pia imechukua Zambia Cup mara 7, Kombe la Barclays ambalo sasa linashikiliwa na Zesco mara mbili .


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic