December 5, 2016





Kampuni ya  StarTimes Tanzania imetoa ufadhili kwa wanafunzi watatu wa chuo cha Sokoine University of Agriculture  katika fani ya Human nutrition ambao wataweza kusomeshwa kwa kipindi chote cha  miaka mitatu.Ufadhili huo umetolewa wakati mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika  Morogoro.

Katika mahafadhali hayo yaliyohudhuriwa na Naibu Waziri Wa Habari,Utamaduni ,Sanaa Na Michezo Mh.Anastazia Wambura ameishukuru StarTimes kwa jitihada zake za kuendelea kuisaidia jamii na hasa katika sekta ya elimu.


Amesema kuwa jamii inakabiliwa na tatizo la utapiamlo na lishe bora hivyo ufadhili huo utasomesha wanafunzi hao ambao wataweza kusaidia kuelimisha jamii juu ya masuala mbalimbali ya lishe na hasa kuonesha umuhimu wa somo hilo katika jamii.

Akizungumza mkurugenzi wa StarTimes Tanzania, Liao Lanfang amesema kuwa Kampuni imekuwa mdau mkubwa wa kusaidia jamii na hasa  elimu hivyo wataendelea kusaidia ili kumuunga mkono mheshimiwa rais katika jitaihada za kuisadia sekta ya elimu.


Akitangaza waliopahatika kupata ufadhili huo Kaimu mkuu wa chuo cha SUA prof. Gerald Monela ametaja kuwa ni Careen Mhegema,Lizy-Mindy Fimbo na Suzan Kikuli. 

Ameongeza kuwa wanafunzi hao wamechaguliwa kutoka na vigezo vikuu vitatu ambavyo ni uwezo wa kitaaluma,fani ya Human nutrition ambapo pia ufadhili huu umeelekezwa kusaidia watoto wa kike.Wanafunzi hao watasomeshwa kwa miaka yote mitatu huku StarTimes ikiahidi kuendelea kusomemsha wengine kwa awamu nyingine tatu.

Ameongeza kuwa kampuni ya startimes imesaini mkataba na chuo na itawalipia mil 3 kila moja kwa mwaka kwa wanafunzi watatu ambapo jumla  itakuwa million 9.Hata hivyo  StarTimes itaendelea kusaidia jamii  ili serikali iweze kufikia lengo la kuwa na wasome  wengi zaidi na wenye ujuzi  ili waweze kukabili soko la ushindani.

Kaimu mkuu wa chuo cha SUA Prof Gerald Monela  ameshukuru  kwa ufadhili huo hasa katika fani zenye uhitaji katika jamii kwani jamii inatakiwa iwe na uelewa wa kutosha juu ya lishe  na SUA inaendelea kuelimisha kutokana na miradi mbalimbali kupitia wadau wake wa lishe na chakula.

Hata hivo kampuni pia iliwazadia wanafunzi bora wengine watatu katika fani mbalimbali ambapo kila moja aliweza kupata dekoda ya StarTimes ili waweze kupata habari na wazidi kujielemisha kupitia channeli bora zenye maudhui mbalimbali.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic