December 3, 2016




Baada ya kusaini miaka miwili kuichexea Yanga, kiungo mkabaji wa timu hiyo, Justine Zulu jana Ijumaa alipewa jezi namba 14 na kuanza mazoezi na wenzake. Jezi namba 14 inatajwa kuwa na mikosi katika kikosi hicho.

Jezi hiyo, ina sifa moja pekee ambayo kila mchezaji mpya atakayeivaa huwa hadumu kwenye timu muda mrefu na badala yake kujikuta anatemwa au kuanza na wakati mgumu.

Kati ya wachezaji waliowahi kuivaa jezi hiyo na kudumu kwa kipindi kifupi ni kiungo mshambuliaji raia wa Niger, Issofou Boubacar aliyedumu na timu hiyo kwa miezi sita pekee kwenye msimu wa 2015/2016, pia beki wa kati Rajab Zahiri aliyeitumikia kwa msimu mmoja na nusu.

Taarifa zinaeleza kwamba, Zulu anayefahamika pia kama mkata umeme kutokana na sifa yake ya uhodari wa kukaba na kuanzisha mashambulizi, yeye mwenyewe ndiye aliyeomba apatiwe jezi hiyo.“Zulu amepewa jezi namba 14 mara tu baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga, ataanza kuonekana nayo kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu.

“Jezi hiyo, yeye mwenyewe ndiye aliyeiomba kabla ya viongozi kumpa na kuanza kuivaa kwenye mazoezi ya leo (jana) jioni kwenye viwanja vya Gymkhana,” alisema mtoa taarifa huyo.

Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh kuzungumzia hilo, alisema: “Hizo taarifa ni za kweli, Zulu nimempa jezi namba 14 aliyoiomba yeye mwenyewe,” alisema Saleh.
Zulu jana jioni alivaa jezi hiyo katika mazoezi ya timu yake kwenye Viwanja vya Gymkhana chini ya Kocha George Lwandamina.

Katika mazoezi hayo, Zulu alionyesha uwezo mkubwa katika kumiliki mpira na kukaba huku akipiga pasi nyingi za visigino kiasi cha kushangiliwa na mashabiki wachache waliokuwepo nje ya uzio wa uwanja huo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic