January 16, 2017







DR Congo imeitwanga Morocco na kuandika ushindi wa kwanza katika michuano ya Afcon 2017 inayofanyika nchini Gabon.

ushindi huo umepatikana kupitia bao la Junior Kabananga aliyefunga katika dakika ya 55.

Hata hivyo, Morocco ndiyo waliokuwa wakishambulia zaidi kuliko DR Congo waliokuwa makini katika kujilinda.


DR Congo walipata pengo baada ya Lomalisa Mutambala aliyeingia katika dakika ya 64 kulambwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu katika dakika ya 85.

Kipa Matambi ambaye ni kipa wa TP Mazembe, alikuwa kikwazo kikubwa kwa Morocco ambao walishambulia zaidi.


Kwa ushindi huo, DR Congo sasa wanaongoza kundi C wakiwa na pointi tatu na kufuatiwa na Ivory Coast, Togo ambao kila mmoja ana pointi moja huku Morocco akiwa anaburuza mkia akiwa hana kitu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic