January 18, 2017



Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga ni baba lao hapa nchini, ni baada ya kuzizidi Simba na Azam FC kwenye orodha ya Klabu Bora Afrika.

Hiyo ni kwa mujibu wa orodha iliyotolewa juzi Jumapili na mtandao mkubwa wa kimataifa wa FootballDatabase.

Kwa mujibu wa orodha hiyo, Yanga inaongoza ubora Tanzania baada ya kujikusanyia pointi 1252 ikipanda kwa nafasi 14 huku ikikamata nafasi ya 332 barani Afrika.

Azam waliochukua Kombe la Mapinduzi hivi karibuni, wenyewe wanashika nafasi ya pili nchini Tanzania kwa pointi zao 1249 na kukamata nafasi ya 353 barani Afrika.

Simba wanafunga orodha ya Tanzania katika nafasi ya tatu kwa pointi zao 1247 katika nafasi ya 358 barani Afrika.

Katika orodha hiyo, Simba ndiyo timu iliyoimarika zaidi kwa kupanda kwa nafasi 38 toka nafasi waliyokuwa mwaka jana.

Mabingwa wa kihistoria Al Ahly wanaendelea kuongoza barani Afrika wakifuatiwa na Esperance de Tunisia, TP Mazembe, AS Vita na Etoile du Sahel wakikamilisha tano bora.

Yanga, inatarajiwa kuiwakilisha nchi katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku Azam ikicheza Kombe la Shirikisho Afrika, Simba wameporomoka kwa kuwa ni muda mrefu sasa hawajashiriki michuano ya kimataifa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic