April 25, 2017




Salaam…
Namshukuru Mungu kwa sasa masuala yangu binafsi ya kifamilia nimeyamaliza na ninaweza kusema kitu, kwanza niwape pole Wanasimba na wapenda michezo kwa haya yaliyonitokea.

Hakika mimi si mtu ninayeamini uonevu, si mtu ninayeweza kunyamaza nikiona haki inaporwa, si mtu mwenye moyo dhaifu wa kuogopa kukosoa pale panapopaswa kurekebishwa, na nitaendelea kubaki hivyo.

Juzi Ijumaa jioni niliambiwa na ofisi yangu imekuja barua tokea TFF, ikiniarifu kuna wito wa kunitaka nifike Karume kusikiliza mashtaka dhidi yangu Jumapili ya juzi  asubuhi.

Wakati huo nilikuwa safarini Zanzibar kutokana na masuala ya kifamilia yaliyokuwa yananikabiri. Ofisi ikachukua jukumu la kuiandikia barua TFF kuomba kusogezwa mbele kwa shauri hilo hadi Jumanne ya kesho kwa kuwa nitakuwa nimerejea Dar es Salaam.

Barua iliwafikia, nami binafsi nikaongea na Alfred Lucas (msemaji wa TFF) na akanijibu ameipokea yeye na imegongwa muhuri na katibu mkuu wa TFF ameishaipata.

Kumbuka hyo ni jioni ya Ijumaa, Jumamosi nikampigia Alfed kuulizia kikao hicho cha kamati kimepangwa lini? Akanijibu atanipa jibu Jumatatu, yaaani jana. Lakini ajabu, juzi hiyo mkasikia mliyosikia. Ni uharaka upi ilionao TFF wa kushindwa kunipa haki ya kusikilizwa?Naona natural justice katika nchi hii haitambuliki? 

Kila mtu anajua, hata wauaji nao pia husikilizwa! Iweje kwa mtuhumiwa ambae anapigia kelele haki ya mwajiri wake? Kuna hoja dhaifu inajengwa kuwa nilipaswa nijibu binafsi barua ya TFF?

Hivi ningewezaje kuijibu barua wakati sikuwepo Dar es Salaam na sikuwa nimeiona? Pia kipi kibaya klabu yangu isiwe na haki ya kunijibia barua? Wakati leo imepokwa haki ya kutokuwa na msemaji?

Wasitake kutuaminisha kuwa TFF hawajui kuwa nilikuwa nazungumza kwa niaba ya ofisi na klabu yangu? nikija sababu za kunifungia nimejiuliza ni kaka yangu huyu Msemwa aliyekuwa anasoma hii hukumu? nimemuona mtandaoni anasoma hukumu ilio kinyume na hati ya mashtaka!

Hati yao ina makosa mengine na hukumu pia nyingine, ni aina ya hukumu katili zaid kwa viwango vya mpira wetu. Ila nawaambia TFF, Haji hajawahi kuwa dhaifu wa moyo, anaweza kuwa dhaifu wa kiwiliwili lakini nna moyo wa Simba.

Ntapambana kwa kiwango cha juu sana, ntadai haki yangu na ya mwajiri wangu kwa viwango na ntaziomba kamati zao zipokee rufaa yangu na kukaa kwa uharaka huu walionifanyia na nipewe haki ya kusikilizwa.

Nisihukumiwe kishabiki wala kwa chuki na nawahakikishia kikao kitakachokaa na kikiweza kunithibitishia niliosema si sahihi na nimeyatunga na yamepotosha ,ntakubali adhabu hata ya kufungiwa maisha kujihusisha na mchezo huu ulionilea na kunisomesha.

Mwisho niwaombe mashabiki wa Simba watulie tukisubiri hizi barua zao, yangu binafsi na ya klabu.
Siku njema


Haji Manara

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic