May 26, 2017



kuna taarifa kuwa, mabosi wa timu ya Randers FC ya Denmark, wapo kwenye mazungumzo na mabosi wa Azam FC juu ya makubaliano ya kumchukua kiungo wao, Himid Mao.

Hatua hiyo imekuja baada ya Himid kufuzu majaribio ya siku 10 aliyoenda kuyafanya katika timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Denmark, mapema mwezi huu.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, amesema kuwa kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na mabosi hao wa Randers baada ya kuwapa habari kwamba kiungo wao amefuzu majaribio yake.

“Tupo kwenye majadiliano na wao, tunasubiri kusikia ofa yao na kama tukikubaliana basi Himid ataenda kujiunga nao kwa sababu wametuambia tayari amefuzu, hivyo mazungumzo yaliyopo sasa ni baina yao na sisi,” alisema Idd.


Naye Kocha wa Azam FC, Aristica Cioaba amesema kuwa kama dili hilo litafanikiwa, basi anamtakia kila la heri kiungo wake huyo.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic